Diaspora sasa kupatiwa vitambulisho
Written by Stonetown (Kiongozi) // 16/10/2012
Na Salma Said, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshauriwa kuweka utaratibu wa kisheria wa kuwapatia vitambulisho wazanzibari wanaoishi nje ya nchi ili kuendeleza uzalendo wao.
Utaratibu huo umetakiwa wende sambamba na kuweka kifungu cha sheria kitakachoweza kumpa uwezo Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi (ZanID) wazanzibari wote ambao hawapo nchini (DIASPORA).
Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma alitoa ushauri huo wakati akiwasilisha maoni na kamati hiyo juu ya Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Mzanzibari Mkaazi ya 2005 na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo mbele ya wajumbe wa baraza hilo linaloendelea Chukwani Mjini Unguja.
Juma alisema kuwatambua wazanzibari waishio nje ikiwa watawawekewa utaratibu maalum nchi itafaidika hasa kwa vile kuna baadhi ya nchi ikiwemo Sirikali na nchi nyengine huchangia pato la taifa kwa kuwekea utaratibu maalum wa kutumia pesa kwa jamaa zao na Serikali kufaidika na kodi kupitia utaratibu huo.
“Kamati yangu inashauri Serikali pamoja kuwa mswaada huu unawalenga wale wakaazi waliopo ZNZ tu lakini ni vyema kikawekwa kifungu cha sheria kitakachoweza kumpa uwezo Mkurugenzi wa Idara ya vitambulisho kuandaa utaratibu maalum wa kuwapatia vitambulisho wale Wazanzibari wanaoishi nchi za nje (DIASPORA) ili na wao wajihisi kuwa wanathaminiwa na Serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar ili wazidishe mapenzi yao kwa nchi yetu na kuondoa zile fikra mbovu kwa nchi yao na Serikali yao na tunaamini itakuwa jambo hili ni chachu ya kusaidia maendeleo kwa nchi yetu. kwani tunawahitaji sana mchango wao wa hali na mali kwa maendeleo ya nchi yetu” Alisema Juma.
Mwakilishi huyo alisema kamati yake inaamini kwamba ombi hilo kwa Serikali litakuwa sio jambo gumu kutekelezwa kwani hivi sasa tayari Serikali imeshaanzisha idara maalum katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi inachoshughulikia na kuratibu masuala ya Wazanzibari wanaoishi nchi za nje (DIASPORA) na pamoja na upya wake lakini kimeanza kazi yake vizuri kwa kuwasiliana na wale Wazanzibari walioko nchi za nje ili kushiriki katika maendeleo ya nchi yao.
Alisema ni lazima wazanzibari wanaoishi nchi za nje kuwapa utambulisho maalum ili kuwajuwa wapi walipo na shughuli zao na kuweza wasiliana nao kwa jambo lolote litakaloweza kuwawezesha wakatoa mchango wao wa mawazo, fikra, busara na hata msaada wa mambo mbali mbali katika serikali yao.
Alisema kuwa ni matumaini yake kuwa ombi hilo kwa Serikali halitakuwa jambo gumu kutekelezwa kutokana na kuwa hivi sasa tayari imeshaanzisha idara maalum katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi inachoshughulikia na kuratibu masuala ya Wazanzibari wanaoishi nchi za nje (DIASPORA), ambayo pamoja na upya wake lakini kimeanza kazi yake vizuri kwa kuwasiliana na wale Wazanzibari walioko nchi za nje ili kushiriki katika maendeleo ya nchi yao.
“Lazima ndugu zetu hawa kuwapa utambulisho maalum ili kuwajuwa wapi walipo na shughuli zao na kuweza wasiliana nao kwa jambo lolote tunalohisi wanaweza wakatoa mchango wao wa mawazo,fikra,busara na hata msaada wa mambo mbali mbali, naamini Serikali yetu itaona umuhimu wa ndugu zetu hawa waishio nchi za nje.
Sambamba na hilo alisema kuwa sheria hiyo inalenga kuwapatia vitambulisho wakaazi wote waliopo Zanzibar wakiwemo wageni wote sio kutoka Bara peke yake lakini hata kutoka nje ya nchi kama vile Italy,Marekani,Ufaransa,Uingereza,Kenya,Uganda,Ghana, hivyo sheria ina nia nzuri na kuwaomba kwa wale wenye fikra potofu au kupotoshwa kuachana na fikra hizo wajue kuwa lengo ni kuwatambua wote.
Chanzo: Mzalendo
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment