Jussa Awajibu
Written by Ghalib // 16/10/2012
Kuna watu (wanajulikana wana kazi zao) ambao wamepend kujifurahisha kuwa Warioba alimbana Jussa na kwamba Jussa alishindwa kujibu hoja zake. Who is Warioba after all? Na kwa hoja zipi za maana alizowahi kuzitoa?
Warioba simply anashindwa kustahamili mawazo yasiyokubaliana na UNYERERE ambao ndiyo itikadi yake na akina Butiku. Alianza kwa kutokubaliana na kile alichokiita mtazamo tofauti wa historia ya uundaji wa Muungano (different perspective on the historical background of the making of the Union) nilipomjibu akakaa kimya! Akataka kujua mifano ya Muungano wa Mkataba na nikamtajia Muungano wa Ulaya (European Union) lakini nikamjibu kuwa Mikataba haina sura moja wala waliokuja na miundo ya Miungano yao ya Mkataba hawana monopoly ya wisdom kuwa lazima tuangalie mifano yao tu akataka kulazimisha mitazamo yake.
Nilipotaka kumjibu Butiku akazuia kwa sababu alijua nitamuumbua. Kilichodhihirik a pale ni kuwa Warioba (ambaye anaonekana amechoka sana hata uwezo wa kufikiri unampungukia) na Ma-Nyerereists wenzake wamepata mshtuko kutokana na wingi (overwhelming majority) wa Wazanzibari wanaotaka Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kufuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba. Anababaika, anaweweseka! Lakini wimbi hili halizuiliki! Wazanzibari tumeamua! Unyerere (ambayo ndiyo itikadi inayowakilisha Ukoloni wa Tanganyika dhidi ya Zanzibar)hauna nafasi tena katika Zanzibar ya leo. Na wachukie wenye kuchukia .Warioba simply anashindwa kustahamili mawazo yasiyokubaliana na UNYERERE ambao ndiyo itikadi yake na akina Butiku. Alianza kwa kutokubaliana na kile alichokiita mtazamo tofauti wa historia ya uundaji wa Muungano (different perspective on the historical background of the making of the Union) nilipomjibu akakaa kimya! Akataka kujua mifano ya Muungano wa Mkataba na nikamtajia Muungano wa Ulaya (European Union) lakini nikamjibu kuwa Mikataba haina sura moja wala waliokuja na miundo ya Miungano yao ya Mkataba hawana monopoly ya wisdom kuwa lazima tuangalie mifano yao tu akataka kulazimisha mitazamo yake.
Nimeitoa habari hii Jamii forum
No comments :
Post a Comment