Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akimuapisha Dk.Juma Malik Akili,
kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,
katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akimuapisha Nd,Ali Khalil Mirza, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makaazi,
Maji na Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Nd,Mussa Haji Ali, kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi,
katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar,leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
(kushoto) akibadilishana mawazo na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad, na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ,
baada ya kuwaapisha Makatibu wakuu wa Wizara mbali mbali na
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa Zanzibar,katika hafla iliyofanyika
Ikulu Mjini Zanzibar.
Dk.Juma Malik Akili,Katibu Mkuu Wizara ya Miundimbinu na Mawasiliano
Ali Khalil Mirza,katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi maji na Nishati
Mussa Haji Ali, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na
Uhujumu wa Uchumi
Dk Shein awaapisha watendaji
wakuu wa Serikali
Na Rajab Mkasaba, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.
Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha baadhi ya Watendaji
viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Shein
alimuapisha Dk. Juma Malik Akili ambaye anakuwa Katibu Mkuu,
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.
Aidha, Dk. Shein amemuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi,
Maji na Nishati Bwana Ali Khalil Mirza pamoja na Bwana Mussa Haji Ali,
ambaye anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa
na Uhujumu wa Uchumi.
Viongozi mbali mbali walihudhuria katika hafla hiyo akiwemo Makamu
wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais
Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi
Mhe. Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Mwinyihaji Makame
pamoja naMwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Utumishi
na Utawala Bora Mhe. Haji Omar Kheir, Waziri wa Miundombinu na
Mawasiliano Mhe. Rashid Seif, Waziri wa Ardhi, Makaazi,
Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban,
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdillahi Jihad Hassan,
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis,
Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib,
Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine.
Mnamo Oktoba 15 mwaka huu Dk. Ali Mohamed Shein alifanya mabadiliko
ya viongozi na watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kutumia
uwezo aliopewa chini ya vifungu vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment