Shivji ataka watu kuchunga ndimi zao kuhusu Muungano
Prof Issa Shivji
Tuesday, 16 October 2012 08:16
Waandishi wetu
MWENYEKITI wa Kigoda cha Mwalimu Profesa Issa Shivji amesema suala la Muungano linapaswa kuangaliwa kwa umakini na kwamba likiachwa kama lilivyo, linaweza kuliingia taifa katika matatizo makubwa.Profesa Shivuji alitoa onyo hilo jana, alipokuwa akizungumza katika mjadala wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa, mjini Iringa.Kauli hiyo ilikuja baada ya wachangiaji wengi katika mjadala huo kutaka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uvunjwe.
“Haya tunayoyajadili ndiyo maneno wanayozungumza wananchi, suala la Muungano lisipuuzwe linapaswa kujadiliwa kwa kina, tusipofanya hivyo madhara yake ni makubwa kwani linaweza kutuingiza kwenye vurugu,”alisema Profesa Shivji.
“Haya tunayoyajadili ndiyo maneno wanayozungumza wananchi, suala la Muungano lisipuuzwe linapaswa kujadiliwa kwa kina, tusipofanya hivyo madhara yake ni makubwa kwani linaweza kutuingiza kwenye vurugu,”alisema Profesa Shivji.
Shivji alionya kuwa suala hilo likiachwa bila kujadiliwa na wananchi wakizuiwa na kutishwa, ili wasijadili Muungano, linaweza kutoa mwanya kwa mataifa yasiyoitakia mema Tanzania kuingia na kuvuruga amani iliyopo.
Akuzungumzia haja na umuhimu wa kuajdili Muungano, Profesa Shivuji alisema kwa hali ilivyo sasa, ni muhimu watu kuujadili hasa ikizingatiwa kuwa muungano wa sasa ulihusha viongozi kwa lengo la kulinda maslahi binafsi.
Mchokaza mada hiyo, alipendekeza wajumbe kujadili kwa kujibu hoja mbili kuhusu namna ya Muungano wanaoutaka na pia kama mchakato wa kuandika katiba mpya una manufaa kwao.
Kuhusu mchakato wa katiba, Profesa Shivji alisema mchakato huo bado unaweza usiwe na matunda kutoka na mafumo muundo wa Bunge maalumu la katiba kutotofautina na ule wa mwaka 1977.
Katika mjadala huo, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Serikali ya Mapinduzi Zanziba, Ibrahim Mzee Ibrahim, aliingia katika malumbano ya kimslahi na mwandishi mkongwe nchini Jenerali Ulimwengu, kila moja akitetea upande wake.
Ibrahimu akizungumza katika mjadala huo alisema kuna ripoti inayoonyesha kuwa maslahi yatokanayo na Muungano ni makubwa kuliko matumizi yake lakini hadi sasa hakuna akaunti ya pamoja iliyoundwa kwa ajili ya kuweka fedha hizo.
“Ingawa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imesema wazi kuhusu kuundwa kwa mfuko wa pamoja na kuwe na akaunti ya kuweka fedha zatokanazo na Muungano lakini hadi leo hakuna kitu hicho, kuna ripoti inaonyesha kuwa mapato yatokanayo na Muungano ni mkubwa kuliko matumizi lakini upande wa bara unakataa kusomwa kwa ripoti hiyo,”alisema Mzee.
Mzee alifafanua kuwa ukiachilia mbali tatizo hilo la kiuchumi, pia kuna tatizo la muundo wa Bunge la kupitisha katiba mpya aliodai halijatofautina na mabunge ya namna hiyo yaliyotengeza katiba zilizopita ikiwamo ya mwaka 1977 inayotumika sasa.
Kwa upande wake, Ulimwengu alikubalina na Mzee juu ya kuwapo kwa fedha katika Serikali ya Muungano, lakini alitetea kuwa bara haiinyonyi Zanzibar.
Katika mjadala huo, Ulimwengu alipendekeza watanzania kuendelea na mjadala juu ya Muungano lengo likiwa kushinikiza viongozi kukubaliana na aina ya muungano wanaotaka.
“Mimi sisemi muungano uvunjwe,kama mpangilio utakuwa mzuri wananchi wa Tanganyika na Zanzibar ni ndugu na wanaweza kunufaika na muungano huo, lakini kama juhudi zote za kuboreha Muunngano zitashindikana basi kama walivyosema uvunjwe itabidi iwe hivyo,”alisema Ulimwengu
Chanzo Mwananchi
No comments :
Post a Comment