VITAMBULISHO VYA KIZANZIBARI
SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR LEO IMEWASILISHA MSWAADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA NAMBA 07 YA MWAKA 2005 YA OFISI YA USAJILI NA KADI ZA VITAMBUSHO ZANZIBAR.
AKIWASILIMISHA MSWAADA HUO KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI KINACHOENDELEA HUKO MBWENI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR MWINYIHAJI MAKAME MWADINI AMESEMA KUWA HISTORIA INAONYESHA KUWA MWAKA 1966 SEREKALI ILIPITISHA SHERIA YAUTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WANANCHI NA WAGENI VILIVYOJUILIKANA KWA JINA LA PASI YA URAIA KWA WANANCHI NA KWA WAGENI PASI YA UKAAZI.
AIDHA WAZIRI HUYO AMESEMA KUWA KUTOKANA NA MATATIZO MBALI MBALI YAKIWEMO YAKIUCHUMI KISIASA NA KIJAMII ,MATUMIZI YA VITAMBULISHO HIVYO YALIONDOKA.
AIDHA WAZIRI HUYO AMESEMA KUWA KUTOKANA NA MATATIZO MBALI MBALI YAKIWEMO YAKIUCHUMI KISIASA NA KIJAMII ,MATUMIZI YA VITAMBULISHO HIVYO YALIONDOKA.
MAPEMA WAZIRI MAKAME AMESEMA KUWA LENGO KUU LAKUANZISHWA OFISI YA USAJILI NA KADI ZA UTAMBULISHO WA ZANZIBAR CHINI YA SHERIA NO 07 YA MWAKA 2005 NI KUWASAJILI WAZANZIBARI WAKAAZI KUTOKANA NA MABADILIKO YAKIUCHUMI NA MAENDELEA YANAYOTOKEA HAPA NCHINI IKIWA NI PAMOJA NAKUANZISHWA KWA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA MASHARIKI,KUONGEZEKA KWA SHUGHULI ZA UWEKEZAJI PAMOJA NA KUIMARIKA KWA SOKO LA UTALII.
KIONGOZI HUYO AMESEMA KUWA MADHUMUNI YA WARAKA WA MSWAADA WA SHERIA HIYO NIKUIFANYIA MAREKEBISHO SHERIA NO 07 YA MWAKA 2005 ILI KUTOA UWEZO KWA OFISI YA USAJILI NA UTOAJI VITAMBULISHO KWA WAGENI WANAOISHI ZANZIBAR.
AMEFAFANUA KUWA HATUA HIYO ITASAIDIA KUKUSANYA TAARIFA BINAFSI ZA WAGENI NAKUHIFADHIWA KATIKA MTANDAO ULIO SALAMA KUHUSU UCHUKUAJI WA ALAMA ZA VIDOLE KWA WALE WOTE WATAKAOSAJILIWA.
NAYE MWENYEKITI WA KAMATI YA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA VIONGOZI WA KITAIFA NDUGU HAMZA HASSAN JUMA AMESEMA KUWA LENGO LA MSWAADA HUO NI KUWEKA UTARATIBU WA UTAMBUZI WA WAKAAZI WA ZANZIBAR NA WAGENI.
AKIWASILISHA MAONI YA KAMATI YAKE AMESEMA KUWA MSWAADA HUO UTARAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA MBALI MBALI KWA WAKAAZI HAO ZINAZOTOLEWA NA MASHIRIKA YA UMMA ZANZIBAR.
MAPEMA WAJUMBE WA KAMATI HIYO WAMEISHAURI SEREKALI KUWEKA KIFUNGU CHA SHERIA KITAKACHOMUWEZESHA MKURUGENZI WA IDARA YA VITAMBULISHO KUANDAA UTARATIBU MAALUM WAKUWAPATIA VITAMBULISHO WAZANZIBARI WANAOISHI NJE YA NCHI ILI KUJIHISI KUWA WANATHAMINIWA NA SEREKALI.
Source: Mzalendo
No comments :
Post a Comment