Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 24, 2012

SMZ KUUZA UMEME KWA SIMU!

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema inakusudia kuanzisha utaratibu wa kununua umeme kwa njia ya simu ili kuwarahisishia wateja wa huduma hiyo…
Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ramadhani Abdalla Shaaban, aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Chukwani Mjini Zanizbar.
Shaaban alisema mazungumzo yanaendelea kati ya Serikali ya Zanzibar na makampuni ya simu ili kuanzisha utaratibu wa kuuza umeme kwa njia ya simu ambayo unaonekana utarahisishia wateja.
Alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuonekana kwamba huduma ya umeme inapatikana katika vituo vya mauzo ambavyo ni vichache katika upande wa Zanzibar na hivyo kusababisha usumbufu kwa wateja wa huduma hiyo.
Waziri huyo ameyasema hayo wakati anajibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Muyuni (CCM), Jaku Hashim Jaku, aliyetaka kujua hatua za Shirika la Umeme (Zeco) kuondoa tatizo la upungufu wa vituo vya mauzo ya umeme mjini na vijiji kwa kuwa imekuwa ni usumbufu wa wananchi wengi kutokana na uchache wake.
Mwakilishi huyo aliiomba serikali na shirika la umeme kuanzisha utaratibu wa kuuza umeme kwa njia ya simu kama ilivyo kwa Shirika la Umeme Tanzania bara (Tanesco) na kwamba utaratibu huo utaondoa foleni katika vituo vichache vilivyopo Zanzibar vya mauzo ya umeme.
Akijibu suali hilo Waziri Shaaban alisema hivi sasa utaratibu huo unaweza kutumika kwa kuwa umeshaonekana unaondosha usumbufu na pia unarihisisha kazi na ndio kukawepo huo mpango.
Waziri Shaaban alisema pamoja na mpango wa kuanzisha utaratibu wa kutumia simu kununua umeme, vituo vya mauzo ya umeme  pia vitaongezwa ili kuwasaidia wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi.
Akitaja vituo hivyo Waziri huyo alisema vituo viwili vipya vya mauzo ya umeme vitaanzishwa ambapo kimoja kitakuwa eneo la Mazizini kwa wakazi wa maeneo ya nje kidogo ya mji wa Zanzibar na chengine kitafunguliwa Vikokotoni kwa wakazi ya Mjini Magharibi.
Wajumbe wengine wa wawakilishi walisema licha ya vituo hivyo vya umeme kuwa vichache kwa Unguja lakini Pemba ndio hali mbaya zaidi ambapo wananchi wengi wanasumbuka sana na upatikanaji wa huduma hiyo.
Mwakilishi wa Konde (CUF), Suleiman Hemed Khamis alisema katika jimbo lake vituo vya mauzo ya umeme vilivyopo Chacke ambako ni mbali kutoka Konde hadi huko kwani ni mkoa mwengine kabisa na kwamba licha ya kuwa mbali  vinafunga mapema, hata wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo wananchi wanasumbuka sana.
Akijibu suali hilo Waziri Shaaban alikiri kuwepo kwa tatizo hizo na kuahidi kuwa kuwasiliana na uongozi wa Zeco kutafuta uwezekano wa vituo hivyo kuongeza muda wa kutoa huduma hadi saa 6 sita usiku badala ya saa nne kama ilivyo sasa.
Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment