Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 16, 2012

TUMEHUSIANA KIDAMU NA WA-OMANI: KIKWETE

Jk Azungumzia Mahusiano Ya Kidamu Na Oman

Pr. Jakaya Mrisho Kikwete

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania na Oman zina mahusiano ya Kidamu na kindugu ambayo ni  maalum sana yanayopaswa kudumishwa, kuthaminiwa na kuenziwa kwa dhati.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemuambia Mfalme Qaboos Bin Said katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika katika nyumba ya kifalme ya Al -Alam mara baada ya kuwasili katika Taifa la Kifalme la Oman jana  tarehe 15.Octoba, kuanza ziara ya kiserikali ya siku 4.
“Tanzania na Oman zina mashirikiano maalum kuliko nchi nyingine yeyote duniani  kwa sababu ya undugu wa damu uliopo baina ya watanzania na wa Oman, hivyo hii ni ziara  maalum sana  katika nchi zetu.” Rais amemuambia Mfalme.
Mfalme Qaboos amekubaliana na Rais Kikwete na kumueleza kuwa ni muhimu mahusiano haya yakadumishwa zaidi kwa njia ya uwekezaji katika nyanja mbalimbali, hasa katika Viwanda.
Rais Kikwete amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula maalum cha usiku ambapo Rais na ujumbe wake wamehudhuria.
Katika ujumbe wake Rais amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof Sospeter Muhongo, Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe. Dr. Abdallah Kigoda, Waziri wa Kazi, Ushirika  na Uwezeshaji , Zanzibar Mhe. Haroun  Ali Suleiman na Naibu Waziri Fedha wa Tanzania Mhe. Janet Mbene.
Katika Ziara hii, Rais amefuatana na wafanyibiashara kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambapo leo tarehe 16 Octoba,2012 atakuwa na kikao na wafanyabiashara wa Tanzania na Oman na hatimaye kutia saini makubaliano ya kibiashara na kiuchumi baina ya nchi mbili hizi.
Mbali na kufanya mkutano na wafanyibiashara, leo Rais  atatembelea makumbusho ya jeshi na jioni  atakutana tena na Mfalme kwa ajili ya chakula binafsi cha usiku.
Mwisho.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Muscat – Oman.
16 Oktoba, 2012

No comments :

Post a Comment