Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 25, 2012

WATU WAPIGWA USIKU!


BENDERA za Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) zimeanza kuteremshwa na kuchukuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi…
Mbali na kuteremshwa bendera watu mbali mbali wamejeruhiwa na vikosi hivyo wakidaiwa kupigwa baada ya kufuatwa majumbani mwao nyakati za usiku na kutakiwa kutoka nje na kupigwa huku baadhi yao wakiwa wamelazwa hospitali wakipatiwa matibabu.
Wakielezea tukio hilo walioshuhudia wamedai kwamba walisikia wakigongewa mlango ya nyumba zao nyakati za usiku na walipotoka wakawakuta watu waliojifunika nyuso zao na kuwataka kuingia ndani na kuanza kupiga watu waliomo ndani mateke, ngumi na vibao hali ambao ilizidisha hofu kubwa katika mitaa kadhaa iliyopo hapa Zanzibar.
“Wamekuja na difender zile za Polisi lakini jambo la kushangaza wamevaa vitambaa vyeusi huwezi kumtambua huyo ni nani lakini gari wanayotumia ni ya Polisi na upigaji wao pia unatambulika kwa sababu wanapiga bila ya kiasi mateke, ngumi, vibao na pia wana vile vifimbo vya polisi,” alidai Bakari Mussa mkaazi wa Alabama Michenzani.
Bakari alisema wana wasiwasi na kuwa wale ni askari wa vikosi pamoja na polisi kwa kutokana na kuwa walikuwa wamebeba silaha za kijeshi mikononi huku viatu walivyokuwa wamevaa ni vile ya Jeshi la Polisi ingawa watu hao hawajavaa sare za polisi lakini wamekuwa wakipita katika majumba na kupiga watu baada ya kuteremsha bendera za Uamsho katika maeneo mbali mbali.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alikanusha jeshi lake kuhusika na matukio hayo huku akisema kazi ya jeshi lake ni kuweka hali ya usalama wa raia na kulinda mali zao na sio kuwatia hofu na kuwapiga.
Akizungumzia suala la kushusha bendera za Jumuiya ya Uamsho Kamishna alisema jeshi lake halihusiki na uteremshaji wa bendera hizo bali wenye kuteremsha bendera ni wenyewe wafuasi wa Uamsho huku akitoa wito kwa wafuasi hao kuwa wataendelea kusakwa na kufikishwa katika vyomvo vya sheria.
“Sisi kama Jeshi la Polisi hatuhusiki na hayo mambo ya kuteremsha bendera na wala hatuhusiki na watu wenye kupita majumbani mwa watu na kupigwa na wala hatuna taarifa hiyo lakini sisi bado tunawatafuta wale wote wanaohusika na vurugu zilizotokea na tutawafikisha katika vyombo vya sheria kwa sababu kuna baadhi yao bado hatujawapata,” alisema Mussa.
Mitaa ambayo imekumbwa na pigapiga hiyo ni pamoja na Mjini Magharibi ikiwemo Michenzani, Mwemberikunda, Saateni, Bububu, Darajabovu, Amaan Wilaya ya Mjini na Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo baadhi ya watu wamesema wameumizwa baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya.
“Wanapachua bendera za Uamsho kila pahala na hilo halina kificho kwa sababu polisi waziwazi tena mchana wanapachua sasa wanaposema kwamba wao hawahusiki basi wanadanganya ulimwengu kwa sababu wanaonekana na kila mtu,” alidai Hamad Issa akiongea kwa njia ya simu kutoka Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment