4th December 2012
NA MWINYI SADALLAH
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka watendaji wakuu wa serikali kutangaza mafanikio na mipango ya serikali ili wananchi waweze kufahamu utendaji wa serikali yao katika shughuli za maendeleo.
Dk. Shein alitoa tamko hilo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kuondoa urasimu wa upatikanaji wa habari unaofanywa na watendaji na wananchi kushindwa kutathmini utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari Uwanja wa ndege wa Zanzibar, Dk. Shein alisema taarifa za mafanikio na mipango ya serikali hazitakiwi kukaa maofisini, lazima zitangazwe kupitia vyombo vya habari ili wananchi waweze kufahamu utekelezaji wa mipango ya serikali.
“Nimewaagiza Mawaziri na watendaji wote wa ngazi zote kutoa taarifa mara kwa mara katika vyombo vya habari, kama kuna viongozi hawataki, mimi nasema hiyo ni bahati mbaya, lakini dhamira ya serikali yangu ni kuweka wazi shughuli zote za maendeleo,” alisema.Dk. Shein alitoa tamko hilo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kuondoa urasimu wa upatikanaji wa habari unaofanywa na watendaji na wananchi kushindwa kutathmini utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari Uwanja wa ndege wa Zanzibar, Dk. Shein alisema taarifa za mafanikio na mipango ya serikali hazitakiwi kukaa maofisini, lazima zitangazwe kupitia vyombo vya habari ili wananchi waweze kufahamu utekelezaji wa mipango ya serikali.
Alisema katika uendeshaji wa serikali, lazima misingi ya utawala bora izingatiwe ikiwamo serikali kufanya kazi zake kwa uwazi ili wananchi waweze kuitathmini, imetekeleza vipi ahadi walizozitoa hasa kwa kuzingatia kuwa wananchi ndiyo waajiri wa serikali.
Dk. Shein alisema safari za nje ya nchi za viongozi wa Zanzibar zimeanza kuzaa matunda, na kupata mafanikio katika uwekezaji, kilimo, uvuvi na elimu, lakini mambo mengi yamekuwa hayaelezwi na watendaji na kusababisha wananchi kuendelea kuamini kuwa viongozi wanatumia fedha nyingi kwa safari za nje.
Alisema kwamba katika kipindi cha miaka miwili, Serikali ya Umoja wa Kitaifa, yapo mambo mengi yamefanyika kama vile ujenzi wa miundombinu ya barabara, serikali kupunguza bei za pembejeo kwa wakulima kwa kiwango cha asilimia 75, ugawaji wa mbolea na mbegu kwa wakulima na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa kushirikiana na serikali za Korea na Marekani.
“Wakati umefika tuache kufanya kazi kwa mazoea, lazima tuwajibike, ili tuweze kujitathmini, tumefanikiwa kwa kiwango gani katika kuongeza uwajibikaji na kujenga misingi mizuri ya uchumi wetu,” alisema Dk. Shein.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment