NA MWANDISHI WETU
8th December 2012
Maadhimisho ya Sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika mwaka huu yanatarajiwa kuwa ya kipekee ambapo viongozi wa Nchi 14 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wahudhuria sherehe hizo.
Kadhalika kwa mara ya kwanza kundi la burudani la sanaa la taifa kutoka Rwanda la ‘the Rwanda National Ballet’ litatumbuiza kwenye sherehe hizo zinazofanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Tanganyika ilipata Uhuru tarehe 9, Desemba 1961 kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza.
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, iliyotolewa jana jijini ilisema Miaka 51 ya Uhuru pia itapambwa na gwaride la halaiki maalumu, makundi ya ngoma kutoka Zanzibar, Ukerewe na Dodoma
Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni 'uwajibikaji,uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa Rais Jakaya Kikwete ndiye mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya kitaifa.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment