Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 14, 2012

Vurugu zatawala mkutano wa CCM

14th December 2012


Jeshi  la polisi mkoani Mara limelazimika kurusha risasi za moto ili kuwadhibiti watu waliodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Musoma mjini ambao walionekana kupinga kauli ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, za kudai kuwa madiwani wa halmashauri hiyo wanatumia vibaya fedha za halmashauri hiyo.

Bulembo ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, alikumbana na hali hiyo juzi jioni wakati akihutubia wanachama wachache wa Ccm katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Mkendo huku mkutano huo ukikumbwa na zomea zomea na kufanya kiongozi huyo kukatisha hotuba yake kila mara.

“Serikali imeleta fedha kwaajili ya kumalizia ujenzi wa ofisi ya Manispaa, madiwani wa Chadema wamehamisha fedha hizo na kuzielekeza kujenga barabara…utaratibu wa kubadili matumizi utawatokea puani siku si nyingi mtakuja kuona,” alisema Bulembo na kuchafua hali ya hewa.

Kutokana na kauli hiyo, vijana,wakina mama na wazee ambao walikuwa enao la karibu na mkutano huo, walianza kuzomea.

Zomea zomea hiyo ilionekana kumkera Bulembo ambaye alisema kuwa hata wakizidi kushangilia vitendo hivyo kwa kipindi kifupi kijacho hawatapata maendeleo kwani serikali hawezi kuleta fedha kwa kulenga mradi wowote kisha madiwani wakahamisha matumizi yaliyokusudiwa.

“Baada ya miaka miwili utasaga meno hakuna fedha mtakazozipata hapa kwa maendeleo na watu watafikishwa mahakamani…mfano mzuri huyu Meya wenu Kisurura ameletewa milioni 96 za barabara, yeye kapeleka milioni 70 na kujenga barabara chini ya kiwango na mitaro hivyo hivyo,” alisema Bulembo huku akiendelea kuzomewa.

Baada ya kuona hali hiyo imekuwa ngumu alijaribu kuhamia kwa Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Godbless Lema, akidai ameshangaa kuona kwa jinsi Lema asivyoheshimu maamzi ya mahakama kwa kitendo chake cha kuandika kwenye kitabu cha wageni nyumbani kwa Mwalimu Nyerere kuwa ni Mbune wa Arusha Mjini wakati akijua siyo mbunge wa Arusha Mjini.

Kauli hiyo ilionekana kuwachukiza zaidi watu hao ambao walikuwa wengi kuliko wale walikuwa wakimsikiliza Bulembo ma kuwatolea maneno ya kuwadukuza eneo  hilo. Baada ya maneno hayo Bulembo aliwaambia waliokuwa wakimsikiliza kuwa akisema CCM oyeee, CCM oyeee, Ccm oyeee’.

Baadaye alisema  kuanzia sasa CCM haitawavumilia tena watu watakapanda katika majukwaa  na kuanza kumtukana na kutoa rugha za kashfa kwa Rais Jakaya Kiwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.

Wakati mkutano ukikaribia kumalizika, polisi walianza kuwakamata ovyo vijana waliokuwa wakiimba jina la Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, jambo lilosababisha baadhi ya vijana kurusha mawe na kuwafanya polisi kurusha risasi na kuwalazimisha waliokuwapo  kukimbia.

Baadaye polisi waliondoka na baadhi ya vijana waliowakamata.


 CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment