WARIOBA AZIDI KUUMIZWA KICHWA ZANZIBAR, AAMINI NI MKATABA TU!
Zanzibar na Tanganyika ndani ya fungamano la MKATABA inawezekana.
Jamhuri ya watu wa Zanzibar Kwanza!!!
Written by Ahmed Omar Khamis // 21/01/2013
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Baba wa Maridhiano ya wazanzibari na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambae ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar, Mhe Amani Abeid Amani Karume leo amekutana na Jaji Joseph Warioba na kuwasilisha maoni yake. Katika maoni yake amesema kwamba wakati wa siku za mwanzoni, Muungano ulikuwa wa heshima na usawa kati ya Zanzibar na Tanganyika lakini kadiri siku zinavyokwenda unachukua sura ya nchi moja -Tanganyika – kuuhodhi Muungano huo dhidi ya Zanzibar. Akasema akiwa Rais kwa kipindi cha miaka 10 ameshuhudia mengi dhidi ya maslahi ya Zanzibar. Alisema hizi ni zama mpya za uwazi na ukweli na kwa hali iliyofikia sasa hakuna njia nyengine zaidi ya kila nchi – Zanzibar na Tanganyika – kurejesha mamlaka yake (sovereignty) kitaifa na kimataifa na kisha nchi hizo mbili kushirikiana kupitia Muungano wa Mkataba kati yao.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment