Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 21, 2013

KATIBA MPYA: katibu wa VIP2 nae awakilisha maoni yao


KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Zanzibar, Dk Khalid Mohamed amependekeza nafasi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Muungano itazamwe upya na kuondoa kero za Muungano.

Dk Mohamed alisema hayo alipotoa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba jana, kwa niaba ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Huku akisisitiza kuwa maoni hayo si msimamo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bali ni maoni ya Watumishi wa ofisi hiyo, alisema Katiba Mpya itazame upya nafasi hiyo ili iwe kama Hati za Muungano zinavyosema.
“Wakati Rais Nyerere (Julius) na Rais Abeid Amani Karume wanakubaliana kuunda Muungano, kuna mambo walikubaliana katika hati hiyo ya Muungano, kwamba Rais Nyerere awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, Abeid Amani Karume kuwa Makamu wa Rais katika Serikali ya Muungano,’’ alisema DK Mohamed.
Dk Mohamed alifafanua kuwa Katiba ya sasa haionyeshi wala kumpa nafasi yoyote Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika masuala ya Muungano, hivyo tumependekeza katika Katiba ijayo nafasi yake itazamwe upya.
Mbali na hilo, Dk Mohamed alisema pia wamependekeza mambo ya Muungano yatazamwe upya katika Katiba ijayo ili kuondoa malalamiko yaliyopo baina ya pande mbili za Muungano.
Alisema kwa sasa mambo ya Muungano yapo 22, lakini kiukweli ni zaidi ya hayo yaliyopo sasa kwa sababu utakuta jambo moja lina mambo mawili au zaidi.
Alisema ili hilo lifanikiwe ni lazima pande zote mbili za Muungano zikutane na kuainisha kwa uwazi ni jambo lipi linalohusu Muungano na mipaka yake ijulikane ili kufanya Muungano uwe imara.
“Kubainisha mambo ya Muungano na mipaka yake ni jambo la muhimu wakati huu ambao tunataka kuandika Katiba yetu, kwa kufanya hivyo tutaweza kupata mifumo ya kikatiba ambayo itasaidia kutekeleza mambo ya Muungano,” alisema Dk Mohamed.
Alisisitiza kuwa ili kufanya Muungano kuwa imara Katiba ijayo iweke vyombo vya kusimamia mambo ya Muungano ambavyo vitakuwa na sura ya kimuungano.
“Sura ya Muungano itakuwepo pale ambapo viongozi na watumishi wa vyombo hivyo vya Muungano watakuwa wanatoka katika pande zote mbili za Muungano na kwa uwiano sawa,” alisema.
Chanzo: Mwananchi

No comments :

Post a Comment