Written by Abdul // 21/01/2013
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, zinaeleza kwamba kiongozi huyo ametoa maoni yake tarehe 13 Januari, 2013 na katika maoni yake ameieleza Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiongozwa na Joseph Warioba kwamba anataka kuona Zanzibar na Tanganyika kila moja ikiwa ni nchi yenye mamlaka kamili ndani na nje na kisha zishirikiane kwa mfumo wa ushirikiano kama ule uliopo baina ya nchi za Afrika kupitia Umoja wa Afrika (AU). Dk. Salmin Amour amesema msingi wa umoja wa nchi za Afrika umetokana na mashirikiano kati ya vyama vya ukombozi chini ya PAFMECA. Akasema Umoja wa Vyama vya Ukombozi vya Afrika Mashariki na Kati (PAFMECA) ulitambua haja ya nchi za Afrika kuungana baada ya uhuru lakini kwa msingi wa kuheshimu mamlaka ya kila nchi (sovereignty) na mipaka yake. Hivyo, akataka mahusiano mapya kati ya Zanzibar na Tanganyika uzingatie msingi huo ambao ndiyo pia uliojenga misingi ya Umoja wa Afrika (African Union). Waliokuwa bado wana mashaka na umoja wa Wazanzibari katika kutaka mamlaka yao kamili naamini sasa watawafahamu Wazanzibari.
Waasisi wawili wazito wa Zanzibar ambao uzalendo wao hauna mashaka, aliyekuwa Katibu Mipango wa ASP, memba wa Baraza la Mapinduzi la mwanzo kabisa mwaka 1964 na Waziri katika Wizara tofauti za Serikali ya Zanzibar na ya Muungano kwa miaka mingi, mwanachama wa CCM mwenye kadi ya uanachama nam. 7, Mzee Hassan Nassor Moyo, na Katibu Mkuu wa mwanzo wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia alikuwa Naibu Waziri katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na katika Serikali ya Muungano na kisha akawa Balozi wa Tanzania nchini Guinea na Ethiopia, Mzee Salim Said Rashid, wamemaliza kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba asubuhi hii. Wote wawili hawakutafuna maneno jinsi Zanzibar ilivyodhulumiwa katika Muungano huu wa kikatiba na wakamalizia kwamba wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani na nje ya nchi itakayofuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika.

Chanzo ni facebook ya ismail juss/MZALENDO
No comments :
Post a Comment