zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 8, 2013

AFRICA SCHOOL HOME - JK azindua shule ya msingi ya kisasa

President Jakaya Kikwete, and founder and director of Africa School Home, Aimee Bessire, unveil a plaque to inaugurate Ntulya Primary School in Mwanza over the weekend. The school has been built under the sponsorship of the US-based Africa School Home. (Photo: Freddy Maro)

NA MWANDISHI MAALUM

8th September 2013


Rais Jakaya Kikwete, amezindua shule ya msingi ya kisasa ya Ntulya ambayo ni zawadi kwa wanakijiji cha Ntulya kutoka kwa Taasisi ya Africa School House ya Marekani.
Pamoja na shule hiyo Rais amezindua huduma za x-ray kwenye hospitali ya wilaya ya Misungwi ikiwa ni shughuli za mwanzo kwenye ziara yake ya siku tano mkoani Mwanza itakayohusisha kukagua na kuzindua miradi na shughuli za maendeleo.
Shule ya Ntulya iliyoko kilomita 47 kutoka mjini Misungwi ina wanafunzi 466 na walimu 11 na ni zawadi ya taasisi hiyo kwa Wanantulya ambako mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dk Aimee Bessire familia yake aliwahi kuishi.
Dk Bessere ambaye alihudhuria uzinduzi wa shule hiyo na mumewe, Mark Bessire waliishi kijijini hapo na kufanya utafiti kuhusu utamaduni wa kabila la Wasukuma.
Shule hiyo ya kisasa iliyojengwa kati ya mwaka 2008 na 2010 imejengwa kwa matofali ya kuchoma na ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa mwaka, wanaosoma kwenye madarasa 11, huku kukiwa na nyumba 10 za walimu na kisima cha maji safi..
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Dk. Bessire ambaye alihutubia kwa ufasaha lugha za Kiingereza, Kiswahili na Kisukuma, alisema shule hiyo imejengwa kwa gharama ya Sh bilioni 1.038, na kati ya hizo Sh milioni 980 zilitolewa na Africa School House, Halmashauri ya Misungwi ilichangia Sh milioni 28 na nguvu za wananchi zilichangia milioni 30.
Taasisi hiyo ya Marekani pia imewajengea wanakijiji hao kituo cha afya kwenye eneo hilo la shule na Dk. Bessire aliwaeleza viongozi na wanakijiji kuwa taasisi hiyo ina mipango ya kujenga shule sekondari ya bweni ya mfano ya wasichana.
Alisema elimu ya watu wazima haijasahaulika na kwamba yataanzishwa madarasa kwenye shule hiyo kwa ajili ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment