zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 15, 2013

CUF yalaani vikali kumwagiwa tindikali Padri

 

Mkurugenzi wa haki za binadamu, habari, uenezi na mawasiliano ya Umma Salim Bimani
Mkurugenzi wa haki za binadamu, habari, uenezi na mawasiliano ya Umma Salim Bimani.
 
Chama cha Wananchi CUF kimelaani vikali mno kitendo cha kumwagiwa tindi kali kwa Padri wa kanisa katoliki Cheju Zanzibar Anselmo Mwang’amba juzi jioni katika maeneo ya Mlandege, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Mkurugenzi wa haki za binadamu habari uenezi na mawasiliano ya Umma Mh. Salim Bimani amesema kuwa matendo ya kihalifu yanazidi kuongezeka siku hadi siku ndani ya Zanzibar bila ya wahusika kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Amesema tukio hili la kumwagiwa tindi kali kwa Padri si la kwanza wala la pili huku jeshi la Polisi likiwa bado halijawashika wahusika wa matukio hayo ambao kwa makusudi wamekuwa na nia ya kuichafua Zanzibar kimataifa.
Ameitaka Serikali SMZ kupitia Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa wanafanya kila jitihada za kuwakamata wahusika na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkono wake na hatimaye kukomesha kabisa vItendo hivi vya kihalifu ndani ya Zanzibar.
Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili waweze kuwashikilia waliohusika na tukio na sio kukamatwa wasiohusika jambo ambapo linaipelekea jamii kujenga picha mbaya na jeshi hilo.
Aidha Mh.Bimani ametoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao kutoa ushirikiano wa kina kwa jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wa matukio haya ya kihalifu.

Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment