zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 3, 2013

Wataka JKU, KMKM kuwa vyombo vya Muungano

NA LEONCE ZIMBANDU

3rd September 2013


Jeshi la Kukuza Uchumi Zanzibar (JKU) na Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) vimetakiwa kujumuishwa na kuwa  miongoni mwa mambo ya Muungano kama ilivyobainishwa kwenye rasimu ya katiba mpya.

Rasimu hiyo imebainisha mambo saba ya msingi kuwapo kwenye uundwaji wa katiba mpya ili  kushughulikia muungano mojawapo kati ya hayo ni suala la ulinzi na Usalama.

Pendekezo hilo lilitolewa na Ibrahimu Chambuso,  mmoja wa wajumbe wa baraza la asasi za kiraia wilayani Bagamoyo (Bangonet), mkoani Pwani.

Alisema ikiwa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) limekuwa la muungno na kuwa chini ya Wizara ya Ulinzi na JKT, hivyo inapaswa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwa chini ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi au Ulinzi.

“Unajua rasimu imeandaliwa vizuri kwa serikali tatu, lakini mtazamo wangu nahitaji serikali mbili, bali mapungufu  yaliyopo yarekebishwe tutapata katiba nzuri,”alisema.

Mwezeshaji wa kongamano la Bangonet, Emanuel Patuka, alisema yeye jukumu lake ni kuchukua mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wakati wa kuipitia rasimu na kuyawakilisha.

Alisema Baraza hilo limejadili mambo mengi ya msingi ikiwa ni pamoja na kupiga kura na kuchagua serikali mbili ziendelee kwa kuwa zitapunguza gharama kuliko kuongeza mzingo usiobebeka.

“Wakati wa kupiga kura kulikuwa na mvutano, wapo waliohitaji serikali tatu na wengine Serikali mbili ambao ndiyo walioibuka kuwa washindi,” alisema.

Katibu Mtendaji wa Bangonet, Leonard Bankuwia, alisema kongamano hilo limehudhuriwa na washiriki 100, kutoka kwenye asasi 50 zilizopo katika Wilaya ya Bagamoyo.

Alisema kwao ni fursa nzuri kukumbukwa kwani kipindi cha miaka ya nyuma, masuala kama hayo yalikuwa yakijadiliwa  na wasomi, wanasheria na wataalamu wengine mbalimbali.

“Hii kwetu ni fursa nzuri, hivyo tunahitaji ushuru wa forodha  kuwa jambo la muungano na  katiba ijayo iruhusu uraia wa nchi mbili ili kukuza uchumi wa Taifa,” alisema Bankuwia.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment