zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 10, 2013

Muswada Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wapita

NA MUHIBU SAID

10th November 2013

  Tume ya Warioba ivunjwe baada ya Rasimu ya Pili
Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013, huku serikali ikiahidi kuwa wengi watakaoteuliwa na Rais kuwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka asasi za kiraia na kidini, watakuwa ni wanawake.
Pia limepitisha kipengele cha kutaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba ivunjwe baada ya kukabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vile vile, limepitisha nyongeza ya idadi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka 166 hadi 201 watakaotoka katika mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi za kidini.
Ahadi ya serikali ya kuwateua wanawake wengi kuwa wajumbe wa Bunge hilo, ilitolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uliowasilishwa kwa hati ya dharura, bungeni jana.
Alisema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Margareth Mkanga, wakati akichangia mjadala wa muswada huo juzi.
Chikawe alisema idadi ya wajumbe hao imetokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya kamati ya ufundi ya vyama vya siasa na ile ya serikali.
Hiyo ni mbali na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao ni 357 na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar 76.
Chikawe alisema kati ya wajumbe 201, nusu watakuwa wanawake na nusu nyingine, watakuwa wanaume.
Alisema kati ya wateuliwa 201, wanawake watakuwa 101 na wanaume 100. “Tutawapa wanawake kipaumbele,” alisema Waziri Chikawe.
Aidha, alisema kamati hizo za kiufundi zilikubaliana pia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi za kidini kupendekeza majina ya watu wanne hadi tisa, ambayo yatapelekwa kwa Rais, naye atateua majina matatu.
“Rais atakaa na vyombo vyake atateua ndani ya mapendekezo ya mashirika na taasisi hizo. Hatateua nje yake,” alisema Waziri Chikawe.
Kuhusu ukomo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walikubaliana ikome baada ya kukabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba. “Makubaliano hayo ni mwafaka wa muda mrefu baina ya vyama na serikali,” alisema Waziri Chikawe.
Hata hivyo, idadi ya wajumbe 201 kutoka mashirika asasi za kiraia na kidini ilipingwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Mnyika alipendekeza idadi ya wajumbe hao ifike hadi 292 ili iwiane na theluthi mbili ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kwa kuwa idadi yao ni kubwa kulinganisha na ile ya wajumbe wa asasi za kiraia.
Mapendekezo hayo yaliungwa mkono na wabunge wa upinzani, akiwamo David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Tundu Lissu (Singida Mashariki-Chadema), lakini ikapingwa na wabunge wa CCM na mawaziri na kusababisha kuzuka mvutano mkubwa wakati wa mjadala wa kupitisha vifungu vya muswada huo Bungeni jana.
Kafulila alihoji kama hoja ya Mnyika ikiungwa mkono itaiathiri nini CCM? Wabunge hao wa CCM ni Ester Bulaya (Viti Maalumu), Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Pindi Chana (Viti Maalumu).
Wengine waliopinga hoja ya Mnyika, ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge).
Wabunge hao wa CCM walisema kwa nyakati tofauti wakati wakichangia mjadala wa kupitisha vifungu vya muswada huo kuwa hawakubaliani na hoja hiyo ya Mnyika.
Walisema hoja hiyo ya Mnyika imetolewa kutokana na hofu waliyonayo wapinzani kwamba, wabunge wa CCM ni wengi, hivyo wanaweza kuliteka Bunge Maalumu la Katiba.
Nchemba alisema kwa hoja hiyo, wapinzani wanajidanganya, kwani siyo Bungeni tu, bali hata kama utaitishwa mkutano wa hadhara, wengi watakaohudhuria watakuwa ni wana CCM.
Bulaya alisema vyovyote itakavyokuwa, kitakachoamuriwa na Bunge hilo kitakuwa ni kwa maslahi ya Taifa na siyo CCM na kwamba, hata wanaCCM kwenye masuala ya Katiba wanatofautiana.
Kutokana na mvutano huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Zima, kuamua ipigwe kura ya kutamka ‘ndiyo’ kuamua ama hoja hiyo ya Mnyika ikubaliwe au isikubaliwe. Hoja hiyo ya Mnyika ilikataliwa na wabunge wengi.
Kipengele kingine, ambacho kilizua mvutano mkubwa kilihusu uhai wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo wabunge wa upinzani walitaka iendelee ikiwa ni pamoja na wajumbe wake wapatao 30 waruhisiwe kuingia katika Bunge Maalumu la Katiba, huku wabunge wa CCM wakipinga.
Lissu alisema kinachoogopwa na CCM kwa Tume ya Mabadiliko ni kutokana na mapendekezo ya Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba, ya kutaka serikali tatu, ambayo alisema ni ‘mwiba’ mkubwa sana kwa chama hicho.
Alisema aliwahi huko nyuma kusema bungeni kwamba, gharama za Tume ni kubwa, lakini akapingwa vikali na wabunge wa CCM wakisema Tume itafanya kazi muda mrefu, hivyo itahitaji gharama kubwa.
Kauli hiyo ilimfanya Spika Makinda kusimama na kumsahihisha Lissu kwamba, alichokisema kipindi hicho kuwa wabunge wengine walimuunga mkono Mnyika, ni Ezekia Wenje (Chadema) na Lissu.
Lukuvi alisema anao ushahidi wa nyaraka na saini kuwa katika kikao baina ya Rais na vyama, waliopendekeza kuwa Tume hiyo baada ya kumaliza kazi yake iondoke ili kuokoa gharama ni CUF, ambao alisema ni washirika muhimu katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment