Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, November 22, 2013

SMZ KUOMBWA KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA VIGOGO WANAOTUHUMIWA KWA UFISADI

Written by  /Mzalendo 

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeombwa kuunda tume kuwachunguza watendaji wake kutokana na kutapakaa kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za umma.
Akichangia hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka 2012/2013 mwakilishi wa jimbo la Dole Shawana Bukheit Hassan amesema tume hiyo itasaidia kujua uhalali wa raslimali za viongozi hao kulingana na mapato yao.
Shawana amesema fedha serikali zinazokusanywa zinaishia mikononi mwa watendaji wa serikali, hivyo kuundwa kwa tume kutasaidia kupunguza ubadhirifu wa mali za umma
Nae mwakilishi wa jimbo la Kojani Hassan Hamad Omar ameiomba serikali kuwajibisha viongozi wanaobainika kufanya ubadhirifu.Akichangia hotuba ya bajeti amesema baadhi ya viongozi wamekua wakionewa muhali kuwajibisha huku wakiendelea kufanya ubadhirifu wa fedha za umma katika sekta za uchumi
Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema itawanyanganya vitambulisho vya Uzanzibari Ukaazi watu na wageni waliopewa vitambulisho hivyo kinyume na sheria.
Nae Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema kabla kufikia hatua hiyo serikali itafanya utafiti ili kujua idadi ya watu hao na wageni waliopewa vitambulisho vya ukaazi kinyume na sheria.
Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi, amesema watendaji waliotoa vitambulisho hivyo kwa kuwapa watu wasiostahiki watachukuliwa hatua kali za sheria kutokana na kutumia madaraka vibaya.
Amesema baadhi ya wageni waliopatiwa vitambulisho hivyo wamehodhi nafasi za ajira zinazostahiki kupewa wazanzibari kwa kujitambulisha wakaazi
Aidha waziri Aboud amesema serikali itaendelea kuwapatia vitambulisho vya ukaazi wazanzibari waliokoseshwa vitambulisho hivyo kwa sababu mbali mbali zikiwemo za kisiasa

Chanzo: Zanzibar islamic news

No comments :

Post a Comment