Na Muhibu Said
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),
Godfrey Simbeye
Wadau wameikosoa sera ya gesi ya mwaka 2013 iliyotolewa na serikali hivi
karibuni,
wakisema haijagusa mambo ya msingi, ambayo yamekuwa yakiyalalamikia
siku zote,
likiwamo la ushirikishwaji wa wazawa katika utafutaji na uchimbaji wa
maliasili hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
(TPSF), Godfrey Simbeye, alisema taarifa za awali walizonazo ni kwamba, upungufu
uliomo kwenye sera hiyo ni kujielekeza kwenye gesi baada ya kuchimbwa na siyo
katika utafutaji na uchimbaji.
Alisema mambo hayo mawili wamekuwa wakiyapigia kelele kutaka serikali ibainishe Watanzania, ambao ni wamiliki wa maliasili hiyo, watashiriki vipi na kwa kiasi gani na kuahidi kuitolea tamko sera hiyo wakati wowote kuanzia sasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema jambo la muhimu sera hiyo ieleweke na kutekelezeka.
Alisema mambo hayo mawili wamekuwa wakiyapigia kelele kutaka serikali ibainishe Watanzania, ambao ni wamiliki wa maliasili hiyo, watashiriki vipi na kwa kiasi gani na kuahidi kuitolea tamko sera hiyo wakati wowote kuanzia sasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema jambo la muhimu sera hiyo ieleweke na kutekelezeka.
Alitoa mfano wa utata uliojitokeza, baada ya Kampuni ya Ophil inayomiliki asilimia 40 ya vitalu vitatu vya gesi pamoja na Kampuni ya British Gas, zote za Uingereza inayomiliki asilimia 20, kuiuzia Kampuni ya Pavilion Energy ya Singapore kwa Dola za Marekani bilioni 1.3 bila ya kuwapo uhakika wa kuilipa serikali kodi.
Profesa Lipumba alisema kampuni hizo zilitiliana saini mikataba mapema na kufanya biashara ya gesi bila ushiriki wa serikali.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema watu wengi, wakiwamo wafanyabiashara, mawaziri na wananchi wa kawaida, wamekuwa wakijadili suala la gesi bila ya kuwa na ujuzi nalo.
Hivyo, akashauri kabla ya yote, uwekwe kwanza mkakati wa kuwawezesha wataalamu wa sekta ya gesi, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma na kwa vyombo vya maamuzi, kama halmashauri na Bunge, badala ya kulumbana.
Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Haji Semboja, alipongeza hatua ya serikali kutoa sera hiyo na kushauri ipitishwe haraka sambamba na kutayarisha mkakati wa utekelezaji, kwa kutunga sheria ya gesi itakayoitafsiri.
Alisema sera inapasa kutambua Katiba ya nchi kwa manufaa ya Watanzania na akashauri kuwapo taasisi za ndani zitakazoshiriki katika umiliki wa vitalu vya gesi, utafutaji, uchimbaji na uendeshaji wa gesi
Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Hussein Kamote, alisema ingawa bado hajaiona, taarifa za awali zinaonyesha kuwa maoni yao mengi yamo kwenye sera hiyo.
Alisema awali, rasimu ya sera hiyo iliwashirikisha wazawa kwenye usambazaji wa gesi, lakini CTI ikapendekeza pia washirikishwe katika utafutaji na uchimbaji.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, alikubalia na yaliyomo kwenye sera hiyo na kusema wenye maoni wayapeleke kwenye kamati ili yaingizwe kwenye sheria ya gesi na kanuni zake.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment