Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, November 22, 2013

Shvji atema moto kuhusu katiba

Na Jacqueline Massano

Mwanazuoni na mwanasheria nguli, Profesa Issa Shivji.
 
Mwanazuoni na mwanasheria nguli, Profesa Issa Shivji, ameuponda utaratibu wa kuwateuliwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) kwa sababu hawawakilishi wananchi bali wanawajibika kwa wafadhili wao.

Vile vile, Profesa Shivji ameuponda mchakato mpya wa katiba na kudai kuwa umehodhiwa na wanasiasa na kwa sababu haujawashirikisha wananchi na kutahadharisha kuwa unaweza kuleta machafuko makubwa nchini. Alitpa kauli hizo jana kwenye kongamano la mchakato wa Katiba mpya la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) chuoni hapo.

Alisema katika Bunge la Katiba, taasisi zisizo za kiserikali zimepewa nafasi ya kuwa wasemaji wa wananchi wakati hawawajibiki kwa wananchi.

Alisema kwa kuangalia idadi ya wajumbe wanaotokana na mashirika yasiyo ya kiserikali wana uwiano sawa na wawakilishi wa mashirika ya wavuja jasho yaani wakulima, wavuvi, wafugaji na wanazuoni.

Alihoji ng’o zinawawakisha nani katika Bunge hilo na mashirika hayo bila ya aibu kujigeuza kuwawakilisha wananchi kitu ambacho siyo sahihi.



CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment