zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 3, 2013

Kigogo wa CCM awapasha mawaziri

NA MWANDISHI WETU

3rd December 2013


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khamis Mgeja
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Khamis Mgeja, amewashauri mawaziri kuacha tabia ya kuzinyanyapaa ofisi za chama hicho wanapokuwa katika ziara za kikazi mikoani kwa kuwa huko ndiko kwenye taarifa mbalimbali za kero za wananchi.

Mgeja ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, ametoa ushauri huo alipokuwa akiwahutubia wanachama na wananchi mkoani Shinyanga wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya mkoa iliyotembelea wilaya zote za mkoa huo kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

Alitoa kauli hiyo Hali hiyo ilitokana na malalamiko yaliyotolewa na wananchi na baadhi ya wana-CCM kulalamikia kero mbalimbali katika maeneo yao ambazo watendaji wa serikali wameshindwa kuzipatia utatuzi zikiwamo zinazopaswa kushughulikiwa kitaifa na wizara husika.

Alisema baadhi ya mawaziri wanaofanya ziara za kikazi mikoani na mawilayani wana tabia ya kukimbilia katika ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya hata pale wanapokwenda katika ofisi za CCM huchungulia mara moja na kuondoka baada ya kuweka saini katika vitabu vya wageni.

 “Binafsi sifurahishwi na tabia hii ya mawaziri wetu kuzigeuza ofisi za CCM kama “mama mkwe”, wengi wao wanapokuwa katika ziara za kikazi wanaishia kupokea taarifa za wakuu wa mikoa na wilaya basi, hawana habari na ofisi za CCM wakisahau kwamba chama hiki ndicho kilichowapa tiketi za nyadhifa walizonazo,” alisema.

“Katika ofisi za CCM ndiko kwenye orodha ya kero za wananchi, baadhi ya kero ni za wananchi kuwalalamikia watendaji wa serikali, hivyo siyo rahisi kwa mkuu wa mkoa au wa wilaya akatoa mbele ya waziri taarifa inayomlalamikia yeye mwenyewe,” aliongeza.

Alisema: “Naamini iwapo watajenga utamaduni wa kufika katika ofisi za chama wataelezwa kero hizo, watapewa ushauri jinsi gani wazipatie utatuzi, lakini pia ushauri wa nini kifanyike katika kuboresha zaidi utendaji ndani ya wizara zao. Pia wataelezwa ni watendaji gani wa serikali katika wilaya ama mkoa wasiotimiza wajibu wao.”

Alisema baadhi ya kero zinapaswa kupatiwa utatuzi wake katika ngazi ya taifa na kutoa mfano kuwa wilayani Kahama lipo tatizo la umeme, hili ni la kitaifa, na kwamba waziri anapokwenda na kuishia kwa mkuu wa wilaya hawezi kupata picha halisi kwani wengi wao hawana utamaduni wa kusikiliza kero za wananchi.

“Mara nyingi kinacholaumiwa ni Chama Cha Mapinduzi, na kero za wananchi zisipopatiwa utatuzi kitakachohukumiwa ni CCM, sasa nawasihi na kuwashauri mawaziri wetu waache kuzinyanyapaa ofisi za chama chao wasikione cha maana nyakati za uchaguzi wanapojipitisha katika ofisi hizo na kumwaga shikamoo kwa kila mtu,” alisema.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment