JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 31 Ogasti, 2014
Taarifa kwa umma: Upepo mkali unaoambatana na mawimbi makubwa vinatarajiwa katika maeneo yote ya ukanda wa Pwani. Taarifa Na. | 201408-02 |
Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki | Saa 6:00 Mchana |
Daraja la Taarifa: | Tahadhari |
Kuanzia: Tarehe | 01 Septemba, 2014 |
Mpaka: Tarehe | 02 Septemba, 2014 |
Aina ya Tukio Linalotarajiwa | Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 inatarajiwa katika ukanda wote wa Pwani. |
Kiwango cha uhakika: | Juu: (70%) |
Maeneo yatakayoathirika | Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. |
Maelezo: | Hali hii inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika maeneo ya kusini mwa Afrika hivyo kusababisha upepo mkali wa Kusi, mashariki mwa Pwani ya Tanzania. |
Angalizo: | Wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari. |
Maelezo ya Ziada | Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi. |
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment