Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania (kushoto)Moezz Mir akimkabidhi
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako,
hundi yenye thamani ya shilingi milioni 48. Kwa ajili ya kuwasomesha
wakunga 10 ambao baada ya kupata elimu wataajiriwa katika vituo vya afya
hasa vijijini ili kuwasaidia akinamama wanaohitaji huduma za uzazi.KCB
na AMREF wametangaza ushirikiano katika kusaidia suala zima la Afya ya
mama na mtoto nchini, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, wapili
kutoka kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB
Christina Manyenye na Meneja msimaizi wa mifuko wa jamii wa Amref
Lilian Nsemwa.( fund Raising Manager).
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Heath Africa Tanzania Dk. Festus Ilako,
akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo
pichani)wakati alipokuwa akiongelea juu ya ushirikiano wao na benki KCB
Tanzania katika kusaidia suala zima la Afya ya mama na motto nchini
.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Moezz Mir na Mkuu wa
Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Christina Manyenye wakimsikiza kwa
makini.
Chanzo: Vijimamabo
No comments :
Post a Comment