airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 27, 2014

Kiwanja Kipya Kariakoo Chafanya Majaribio yas Pemba Zake leo na kuvurika watoto wengi kupanda pembea hizo.

 Wananchi wakiwa na watoto wao wakiingia katika kiwanja cha watoto kariakoo wakati wa majaribio ya mapembea yalioko katika kiwanja hicho baada ya kufungwa kwake karibu miezi mitatu kupita ili kutowa huduma kwa watoto wakati wa kusherehekea sikukuu ya Eid Alhajj inayotarajiwa kuadhimishwa mwishoni mwa wiki ijayo kuungana na Waumini wa dini ya kiislam baada ya kumalizika kwa Hijja inayofanyika nchi Saud arabia.
Meneja Mipango, Uwekezaji na Utafiti Ndg, Khalifa Muumin, akiwa katika moja ya pembea katika kiwanja hicho kuangalia utowaji wa huduma kwa watoto waliofika katika kiwanja hicho leo jioni wakati wa majaribio ya pembea zake kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya eid alhajj., kuona kama kuna matatizo katika pembea hizo. 

Pembea ya gari ziendazo kasi 
                                                   Pembea ya kikapu hiyooo ..........
Pembea ya vibesi ikitowa burudani kwa watoto waliofika kiwanjani hapo wakati wa majaribio yake leo jioni
                                                          Pembea ya farasi wawaaaaaaa
              Pembea ya ndege ikiruka wakati wa majaribio ya pembea hizo.mpya
Meneja Mipango, Uwekezaji na Utafiti Ndg, Khalifa Muumin na Afisa Uhusiano wa ZSSF Ndg, Mussa Yussuf wakiwa katika kiwanja cha watoto kuangalia hali ya majaribia hayo ya mapembea  mapya yaliofungwa kwa ajili ya kuchezea watoto wanaofika kiwanjani hapo ikiwa ni majaribio kwa ajili ya maandalizi ya kusherehekea sikukuu ya Eid Alhajj inayotarajiwa kuadhimishwa hivi karibuni. 
 Wazazi wakiwa na watoto wao wakiingia katika viwanja vya watoto kariakoo kushuhudia majaribio ya pembea hizo,
Pembea ya miavuli ikiwa katika kiwanja cha watoto kariakoo, ikiwa katikac majaribio yake baada ya kazi za kuzifunga kumalizika ili kuona ubora wake. 
Pembea ya kisasa ya kwenda kwa kasi juu ikitowa burudani kwa watoto waliofika kiwanjani hapo wakati wa majaribio ya mapembea hayo kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya Eid Alhajj mwishoni mwa weiki ijayo.

Pembea ya mfano wa jahazi wakibembea watoto kiwanjani hapo wakati wa majaribio ya mapembea hayo baada ya kufungwa kiwanjani hapo kutowa burudani kwa watoto.

               Moja ya pembea za kisasa katika kiwanja cha kufurahishia watoto kariakoo
Watoto wakiwa na furaha wakisubiri kupanda moja ya pembea katika kiwanja hicho kipya cha watoto kariakoo.
Watoto wakifurahia pembea za gari wakati wa majaribio ya pembea hizo yaliofanywa na mmiliki wac Kiwanja hichoMfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF. 
Watoto wakiwa nje ya uwanja wa watoto kariakoo wakisubiri kuingia ndani kupanda pembea katika uwanja huo leo jioni wakati wa majaribio ya pembea hizo.

Chanzo: ZanziNews 

2 comments :

  1. hili tangazo la "YOU MAY ALSO LIKE...." LIWEKENI VIZUR TUNASHINDWA KUSOMA BAADHI YA TAARIFA AU LIWEKEENI BATAN YA KUKANSELI.

    ReplyDelete
  2. hili tangazo la "YOU MAY ALSO LIKE...." LIWEKENI VIZUR TUNASHINDWA KUSOMA BAADHI YA TAARIFA AU LIWEKEENI BATAN YA KUKANSELI.

    ReplyDelete