Na Laylat Khalfan
TANI 14.35 za majongoo ya
pwani, zimesafirishwa nje ya nchi kwa
mwaka 2013.
Akizungumza na mwandishi wa
habari ofisini kwake Maruhubi, Mkuu wa kitengo cha usarifu na ukuzaji wa masoko,Hamad
Khatib, alisema kiwango hicho kimeshuka ikilinganishwa
na tani 21 zilizosafirishwa mwaka 2012.
Alisema sababu za kupungua usafirishaji
majongoo ni upungufu wa mazao hayo kutokana na kuongezeka idadi ya wavuvi.
Alisema soko kubwa la majongoo
ya Zanzibar ni Marekani,Korea, Honkong, Vietnam, Dubai na nchi nyengine za
Ulaya.Kwa upande wake, Hashim Muumin
ambae ni Mtafiti wa mazao ya baharini,
alisema majongoo yapo hatarini kutoweka kutokana na kuongezeka idadi ya wavuvi.
Aidha alisema ipo haja kwa serikali
kuweka mikakati madhubuti ili kuunusuru
uvuvi huo.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment