Na Daniel Mjema, Mwananchi
“Wanaume wana haki ya asili kuanzia kwenye biblia,
ndio maana wanaambiwa wao ni kichwa cha familia. Sasa tunadaije haki
sawa na wanawake?” alihoji Nyangwine.
Dodoma. Mjumbe wa Bunge la Katiba, Nyambari
Chacha Nyangwine amewapiga vijembe wanaume wanaotaka haki zao ziingizwe
kwenye Katiba.
“Wanaume wana haki ya asili kuanzia kwenye biblia,
ndio maana wanaambiwa wao ni kichwa cha familia. Sasa tunadaije haki
sawa na wanawake?” alihoji Nyangwine.
Mjumbe huyo alitaka wajumbe wenzake kupigania haki
za msingi za wanawake kama usawa katika vyombo vya maamuzi ili
ziingizwe kwenye Katiba.
Wiki iliyopita wajumbe walio wachache katika
Kamati Namba Tisa ya Bunge, walipendekeza wanaume wanaopigwa na wake zao
nao walindwe katika Katiba mpya.
Mapendekezo hayo yaliyowaacha hoi kwa kicheko,
yaliwasilishwa na mjumbe wa kamati hiyo, Mbaraka Hussein Igangula kwa
niaba ya wajumbe walio wachache.
“Kwa mfano kuna baadhi ya wanaume wamekuwa
wakipigwa na wake zao na kunyang’anywa mali kutokana na sababu
mbalimbali,” alisema na kuwafanya wajumbe kuangua kicheko.
No comments :
Post a Comment