Wadau
mbalimbali wa madini ya vito waliopata bahati kutembelea Banda la
Tanzania katika siku ya kwanza ya Maonesho ya 54 ya Kimataifa ya Vito na
Usonara ya Bangkok, wakishangazwa na mng’ao wa Kito cha Tanzanite
katika Pete iliyovalishwa kidoleni mwa Mwanafunzi, Raia wa Thailand
aliyeomba kujaribisha Pete hiyo. Anayetoa maelezo ni Mfanyabiashara wa
Madini ya Vito kutoka Tanzania, Bw. Gregory Kibusi (Mwenye mavazi ya
Bhatiki).
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya
Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo akizungumza na mdau wa
madini ya vito aliyetembelea Banda la Tanzania. Kalugendo alitumia fursa
hiyo kumkaribisha mdau huyo katika Maonesho ya Vito ya Arusha
yanayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu nchini Tanzania.
Katikati ni Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Asimwe Kafrika.
Sehemu
ya shehena ya madini mbalimbali ya vito katika Banda la Tanzania kwenye
Maonesho ya 54 ya Kimataifa ya Vito na Usonara ya Bangkok.
Wafanyabiashara
wa Madini ya Vito kutoka Tanzania, Gregory Kibusi (Mwenye nguo za
Bhatiki) na Kassim Iddi Pazi (Mwenye Shati la rangi ya Bluu),
wakimwonyesha Mteja aina mbalimbali za madini ya vito yanayopatikana
Tanzania.
Mgeni
Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 54 ya Kimataifa ya Vito na Usonara
ya Bangkok, ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Thailand,
Bi. Chutima Bunyapraphasara, akikata utepe kuzindua rasmi Maonesho hayo.
Kushoto kwake ni Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito
wa Thailand, Bw. Somchai Phornchindarak na Kulia kwake ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Idara ya Uhamasishaji Biashara Kimataifa, Bibi Nuntawan
Sakuntanaga.
Chanzo: Vijimambo
No comments :
Post a Comment