Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 10, 2015

BoT kutatua migogoro ya wateja, benki

BoT 
KWA UFUPI: Ni baada ya kugundua kuna mitafaruku inayochukua muda mrefu kuisha
Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeanzisha kitengo maalumu kitakachoshughulikia malalamiko na migogoro baina ya wateja na taasisi za fedha nchini, zikiwamo benki.
Naibu Gavana wa BoT, Lila Mkilla alisema hayo jana alipozungumza na wadau wa taasisi za fedha nchini.
Alisema ili kufanikisha mpango huo, BoT imeamuru kila taasisi za fedha nchini kuwa na kitengo maalumu kitakachokuwa kikishughulikia matatizo ya wateja wake na endapo mteja hatokubaliana na uamuzi husika, anaruhusiwa kwenda BoT kulalamika.
“Tumegundua katika miaka ya hivi karibuni, kuna ongezeko kubwa la migogoro kati ya wateja wadogo na benki, tunapokea barua nyingi = kutoka kwa wadau wa taasisi za fedha. Wengi wanapata matatizo na kushindwa kujua pa kukimbilia,” alisema Mkilla.
Katibu wa BoT, Yusto Tongola alisema wateja watakaokuwa wakishughulikiwa migogoro yao ni wale wenye miamala isiyozidi Sh15 milioni.
“Awali, wateja walikuwa wakipata shida sana, utakuta muamala wake hauzidi Sh 2 milioni, lakini benki inamzungusha na kuamua kukimbilia mahakamani... wengi tunajua mfumo wa mahakama zetu, kesi zinachukua muda mrefu lakini pia mteja anatumia fedha zaidi,” alisema Tongola.
Tongola alisema mfumo huo ambao pia upo Ghana, Nigeria na Afrika Kusini, utakuwa wazi kwa kila mmoja na utatatua matatizo ya wateja ndani ya siku 90.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa BoT, Slivester Kasikila alisema mfumo huo utasaidia kupunguza malalamiko ya wateja na kuongeza ufanisi katika kazi zao tofauti na awali.
Alisema kipindi cha nyuma wateja waliokuwa na migogoro na benki walipoteza muda mwingi mahakamani.
“Wakati mwingine elimu tu inatosha kupunguza migogoro, BoT sasa itatumika kama rufaa na itatuweka katika mstari,” alisema Kasikila.

No comments :

Post a Comment