Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 10, 2015

Chadema yambwaga zitto Kabwe Mahakamani

Zitto Kabwe
KWA UFUPI: Katika Hukumu Mahakama hiyo imemuamuru Zitto Kabwe kulipa gharama zote za kesi hiyo baada ya kujiridhisha kuwa hakufuata kanuni za kufuangua kesi dhidi ya chama chake.
Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama wake ndani ya chama hicho.
Mahakama hiyo imekubaliana na hoja pingamizi toka chadema dhidi ya kesi hiyo kwamba ilifunguliwa bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Katika Hukumu Mahakama hiyo imemuamuru Zitto Kabwe kulipa gharama zote za kesi hiyo baada ya kujiridhisha kuwa hakufuata kanuni za kufuangua kesi dhidi ya chama chake.
Aidha Mahakama imeamua katika hukumu yake kuwa Chama kinaweza kuendelea na taratibu zake kama jinsi zilivyokuwa zikiendelea kabla ya kuwekwa zuio.
Siku za hivi karibuni Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam ilitoa zuio la muda kwa kamati kuu ya Chadema kutojadili uanachama wa aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe katika vikao vyake.
Januari mwaka jana Mahakama hiyo ilisikiliza hoja za mawakili wa pande zote kuhusu maombi hayo chini ya Jaji John Utamwa , Mahakama hiyo ilitoa zuio la kutojadiliwa kwa uanachama wa Zitto Kabwe hadi hapo kesi yake ya Msingi itakaposikilizwa.

No comments :

Post a Comment