Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 25, 2015

Warioba: Tunahitaji rais mzalendo


Jaji Joseph Warioba 
  • Wataka achukie rushwa kwa vitendo, wasema asijifanye mwadilifu bali awe mwadilifu kwa asili yake.
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Joseph Warioba, ametaja sifa za rais ajaye kuwa ni uzalendo, uadilifu na dira katika kuliongoza taifa.
Jaji Warioba alisema hayo juzi, katika Kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa hewani na ITV.
“Rais anapaswa pia kujua matatizo ya Watanzania, awe mzalendo, mwadilifu na aone mbali. Anapaswa pia kujua  atafanya nini kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta za afya na uchumi,” alisema.
Kwa kauli hiyo, Jaji Warioba anaungana na viongozi wengine kadhaa waliowahi kuzungumzia sifa za rais ajaye, akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk Hassy Kitine; Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye; Mwanasiasa mkongwe, Cleopa Msuya; Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba;  na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao walitaja sifa hizo za rais ajaye kuwa ni uadilifu, busara, uzalendo, uwezo wa kufanya uamuzi na kuyasimamia, weledi wa masuala ya maendeleo, kutokuwa na makundi, kuwa na nguvu ya mwili na akili na uwezo wa kusimamia Katiba na sheria za nchi.
Walisema yeyote asiyekuwa na sifa hizo, hafai kuwa rais na kuwaongoza Watanzania.
Dk Kitine: Urais siyo lelemama
“Mtu anayetangaza (mwenyewe) kuwa anataka kuwa rais anakuwa hajui anachokisema..., anakuwa hajui matatizo ya urais. Mtu asiyejua matatizo ya urais anaweza kujisemea tu kwa sababu haelewi urais maana yake ni nini,” alisema aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na Waziri wa kwanza wa Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Dk Hassy Kitine.
Kitine alisema hayo Septemba 9 mwaka jana. Alisisitiza, “Mtu anayejua maana na changamoto za urais hawezi kutangaza anautaka urais. Ataogopa kwa sababu ya changamoto (nyingi) za urais…, kwa hiyo hawezi kujitangazia ovyo kuutaka.”
 Kwa mujibu wa Dk Kitine anayetaka kuwa rais lazima awe mwadilifu wa asili na siyo wa kujifanya. Awe pia mzalendo na mwenye uwezo wa kufanya uamuzi.
“Rais awe amesoma na asiwe na kundi, pia ajue misingi ya utawala bora, utawala wa sheria na aonekane kuwa anachukia rushwa kwa vitendo. 
Kauli ya Msuya
Mwezi huohuo wa Septemba mwaka jana, mwanasiasa mkongwe nchini, Cleopa Msuya, alitaja sifa 16 za rais ambazo ni pamoja na uadilifu, uzalendo, mpambanaji dhidi ya rushwa na ufisadi na mwelewa na msimamizi wa uchumi.
Sifa nyingine kuwa na shauku ya ustawishaji wa uchumi na uelewa wa kujua umuhimu wa kujenga na kusambaza huduma za miundombinu ya kiuchumi na kijamii. Pia rais anapaswa awe ni mtu mwenye kujua umuhimu wa watu kufanya kazi, uwezo wa kuwatetea na kukomesha unyanyasaji wa wananchi ndani ya nchi yao, uwezo wa kuelewa misingi ya uchumi wa taifa na uwezo wa kufumua maovu yanayofanyika.
Awe pia mnyenyekevu na mapenzi kwa taifa na wananchi,  awe na uwezo kuongoza na kuona mbele, awe na uwezo wa kutofautisha mambo ya nchi na binafsi, aweze kutofautisha mambo ya biashara na mali za umma, kutofautisha mambo ya ofisi na nyumbani na pia awe na uwezo wa kusimamia na kuwezesha wananchi katika uchumi.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/2664832/-/item/1/-/yglxttz/-/index.htm
l


  • HII MAANA YAKE KIKWETE HAKUA MZALENDO.WATU WALIMCHAGUA TUU KWA KUWA ALIPITISHWA NA CHAMA CHAKE.NAFIKIRI PIA CHAGUZI 2010 ILIKUWA IMECHAKACHULIWA .KIKWETE HAKUSHINDA LAKINI NJAMA TUU.KIKWETE HAJA FANYA LOLOTE KWA WANANCHI NA HATA KWA NCHI YETU.WAKATI WAKE KASHFA NA RUSHWA NYINGI ZIMEIBULIWA LAKINI HAMNA LOLOTE KILICHO FANYIKA.NASHANGAA AMEPEWA DEGREE YA DR NA TUZO MBILI AU TATU YA NINI?WAKATI HAJA FANYA LOLOTE.DHULUMA NA UNYANYASAJI PIA IMEZIDI KWENYE NCHI YETU KUTOKA HAWA POLISI NA MATRAFFIC.HAO NDIYO WAMEPEWA NGUVU ZA KUWATESA WANANCHI.
    •  
      • Avatar
        UZALENDO,ni kitu cha msingi tunachohitaji sasa kwa ustawi wa nchi yetu.kuna watu wanaotaka uongozi ili watuuze pamoja na nchi yetu kwa makampuni makubwa kupitia mikataba ya kidanganyifu ya uwekezaji.watu hawa watatweza mtu na vyama vyao dhidi ya maslahi makubwa ya wananchi na nchi yetu tanzania.hawa hawajari vizazi vya kesho katika mahamuzi yao na mipango yao ya kupata uongozi.tafadhali,tuwagundue na tusiwashabikie na kushiriki uhani wao.
          • Avatar
            Mgombea urais anaombwa kugombea na watu "walioteuliwa." Kila chama cha siasa (kama ilivyo kwa vyama vyovyote vingine) kina watu "wateule,' walioteuliwa kwa misingi ya chama husika. Hawa kimsingi ni weledi, waadilifu, wenye busara na wasio na hamaki. Wananchi tunaombwa tumchague mmoja wao kupitia kura ili aiongoze nchi. Watu au vikundi vya watu vinapomwomba mtu kugombea huku vikifahamu kuwa muombwa ni mwanachama katika chama ambacho kina wateule wa kumwomba mtu kugombea vinafanya makosa. Kwa maana nyingine vinadharau mfumo uliowekwa ndani ya chama husika kumpata mgombea. Kwa mfumo huu nadhani tutapata mgombea asiye sahihi, kwa sababu hii mfumo huu wa ugombeaji utaendelea hatimaye kuigaragaza nchi! Mchango wa Mzee Warioba ni mkubwa na wa maana sana, na asichoke kuiasa nchi pamoja na madudu yote yanayoendelea kutengenezwa na wanasiasa wakongwe walionyimwa busara dira na dhima.
              • Avatar
                Kisa ukawa waliliona hili tangu mwanzo ndio mana CCM wanakufa na tai shingoni. Wanadhani wakikubali kuwa kiukweli muda hautoshi watakuwa wamewapa wapinzani wao credit. Tabia hii siyo IGNORANCE bali ni FOOLISHNESS.

              No comments :

              Post a Comment