Makinda alisema hayo alipokuwa akiwajibu wabunge wa upinzani waliolalamika kuburuzwa baada ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, kuomba majibu kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu kura ya maoni.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi a CUF Taifa, Abdul Kambaya, alisema kauli hiyo ya Makinda ni ya dharau, ambayo hazipaswi kutolewa, hasa na kiongozi wa wabunge.
“Spika Makinda anakuwa chanzo cha vurugu bungeni, hasa kwa kuwa mtetezi wa serikali bungeni, badala ya kuwa kiongozi wa Bunge asiyeegemea upande wowote,” alisema Kambaya.
Alisema kitendo cha Spika Makinda kulazimisha kusomwa miswada miwili kuhusu habari na matumizi ya mitandao ya kijamii, hakikubaliki kwa Watanzania na kinadhihirisha kishachoka kuliongoza Bunge.
Alisema kitendo cha Spika Makinda kulazimisha kusomwa miswada miwili kuhusu habari na matumizi ya mitandao ya kijamii, hakikubaliki kwa Watanzania na kinadhihirisha kishachoka kuliongoza Bunge.
“CUF tunamuonya Spika Makinda aache ukada wa CCM na kuiegemea serikali wakati maslahi ya wananchi yanavunjwa na kukanyagwa,” alisema Kambaya.
Alimtaka Spika Makinda kutambua kuwa iwapo ataendelea na utaratibu huo, atalivuruga Bunge na kutowesha amani.
“Anapaswa kutenda haki na usawa kwa wabunge wote bila kujali chama. Na endapo Bunge limemshinda, aachie wanaoweza kuongoza,” alisema Kambaya.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment