zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 19, 2015

Dk Shein ahutubia Baraza la Eid

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipokea saluti ya Gwaride rasmin la Kikosi cha FFU lililoandaliwa kwa ajili ya baraza la Eid katika viwanja ya hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Kilosi cha Jeshi la Polisi FFU kikitowa heshima kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja wa Hoteli ya Bwawani kuhutubia Barza la Eid katika Ukumbi wa Salama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh O,ar Saleh Kabi, alipowasili katika ukumbi wa hafla ya Baraza la Eid Bwawani.kulia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Shekh Abdi Sinani akisoma Quran Tukufu kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya Baraza la Eid lililofanyika katika ukumb wa Salama Bwawani Zanzibar leo. 
Viongozi wa Meza Kuu wakisikiliza Quran ikisomwa wakati wa hafla hiyo wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, 
Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakisikiliza Quran iliokuwa ikisomwa na Shekh Abdi Sinani wakati wa ufunguzi wa hafla ya Baaza la Eid 
Wananhi waliouhudhuria hafla ya Baraza la Eid Mubaraak wakiwa katika ukumb wa Salama
Waziri wa Katiba Sheria Zanzibar Mhe Abubakar Khamis Bakari akimkaribisha Rais wa Zanzibar Dk Shein kulihutubia Baraza la Eid katika Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar 
Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia Baraza la Eid Mubaraak katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli Zanzibar.
Viongozi wa meza kuu Mama Fatma Karume, Mama Mwanamwema Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamah na Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Omar  Saleh Kabi, wakifuatilia Hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiisoma katika Baraza la Eid lililofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
























STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                       18 Julai, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza tena kuwa jukumu la kuhimiza utiifu wa sheria, kusimamia amani, utulivu na usalama wa nchi ni la kila mwananchi wakiwemo viongozi wa kisiasa, taasisi, madhehebu ya dini na viongozi wa kijamii.
“…suala la utii ni muhimu kwa vile humuepusha mtu kuepukana na matatizo yasiyo ya lazima … hivyo tuna wajibu wa kutii Sheria na Katiba ya nchi yetu pamoja na mamlaka inayotuongoza kwa faida ya kila mmoja wetu” alieleza.
Akizungumza katika Baraza la Idd El Fitri lililofanyika katika Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar leo, Dk. Shein aliwaambia waumini waliohudhuria Baraza hilo kuwa serikali kwa upande wake itaendelea kuhakikisha kuwa inaongozwa kwa kuzingatia Katiba na utii wa sheria bila ya kumbagua au kumuonea mtu yeyote.
Dk. Shein aliwasihi wananchi kuyadumisha mafunzo waliyoyapata wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo waumini walionesha uchamungu, utii, subira, usawa mbele ya Mwenyezi Mungu, walihurumiana na kupendana pamoja na kusaidiana katika mambo ya kheri.
“kwa hivyo ni wajibu wetu tuyatumie mafunzo hayo ili tuendeleze utamaduni wa kutenda mambo mema katika maisha yetu ya kila siku pamoja na kujiepusha na makatazo ya Mola wetu ili tuweze kudhihirisha kuwa tumehitimu ipasavyo”  Dk. Shein alieleza.
Katika hotuba yake hiyo, Dk. Shein alizipongeza taasisi za kidini kwa kutekeleza majukumu yao kisheria na wajibu wao kwa jamii pamoja na ushirikiano wao mzuri na serikali.
Alitoa shukrani maalum kwa Ofisi za Mufti wa Zanzibar, Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana pamoja na Ofisi za Makadhi kwa ufanisi waliouonesha katika kutekeleza majukumu yao katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Dk. Shein aliwahimiza viongozi na watendaji serikalini kuendelea kuwatumikia wananchi kwa bidii ili kuwaletea maendeleo na kuwakumbusha haja ya kuzingatia sheria za nchi, kanuni na taratibu zilizwekwa katika utendaji wao.
Kuhusu utekelezaji wa shughuli za kisiasa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alisisitiza kauli yake ya kuwataka viongozi wa vyama kufanya siasa kwa kuzingatia Sheria zilizowekwa na kufuata maadili ya vyama.
“Wanasiasa ni vyema tukakumbushana kwamba ni jukumu letu kushindana bila ya kugombana. Tunaweza kushindana bila ya kukejeliana na tunaweza kushindana bila ya kudharauliana na kuhasimiana” Dk. Shein alisema.
Alifafanua kuwa vyama vya siasa vimeundwa kwa lengo la kushindanisha sera na kuchochea maendeleo na kwamba mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo chini ya mfumo wa Umoja wa Kitaifa ni kielelezo thabiti kueleta amani na maendeleo yanayokusudiwa.
Kwa hivyo wakati huu tukielekea Uchaguzi Mkuu alitoa wito kwa wananchi hasa vijana kuzingatia kauli za viongozi wao za kuendeleza amani na utulivu uliopo nchini na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Dk. Shein alizishukuru pia taasisi mbalimbali kwa huduma zao ambazo zilisaidia kuwafanyia wepesi wananchi kutimiza ibada hii ya funga.
Sambamba na shukrani hizo aliwapongeza na kuwashukuru pia viongozi wa dini ambao walifanya kila juhudi kutoa elimu na mawaidha katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku akiwasihi kuendelea na huduma zao kwa wananchi bila ya kuchoka katika miezi mingine ili kuendeleza mafunzo yaliyopatikana katika mwezi wa Ramadhani.
Mapema Mheshimiwa Rais alihudhuria sala ya Idd iliyofanyika katika viwanja vya Maisara na baadae kwenda Ikulu ambako alipeana mkono wa Eid na viongozi wa dini ya kiislamu, viongozi wa serikali pamoja na wananchi mbalimbali na watoto waliofika Ikulu kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitri.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 
          Chanzo: Zanzinews                                     

No comments :

Post a Comment