Dk. Shein aliyasema hayo jana wakati wa mazungumzo na Balozi wa India nchini anaemaliza muda wake, Debnath Shaw, Ikulu mjini Zanzibar.
Dk. Shein aliipongeza Serikali ya India kwa hatua yake ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta zake za maendeleo.
Alisema Tanzania ikiwemo Zanzibar zina uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na India ambao umeanzishwa na waasisi wa nchi hizo akiwemo marehemu Julius Kambarage Nyerere na waasisi wa nchi hiyo akiwemo marehemu Indira Gandhi.
Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar inathamini uhusiano na ushirikiano kati yake na India hatua ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuwepo ushirikiano katika sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya, biashara, viwanda na sekta nyingine.
Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar inathamini uhusiano na ushirikiano kati yake na India hatua ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuwepo ushirikiano katika sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya, biashara, viwanda na sekta nyingine.
Dk. Shein alitoa pongezi kwa India kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta zake za maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano wake katika kuanzisha chuo cha amali katika kijiji cha Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja ambacho wakati wowote kitazinduliwa.
Utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa chuo hicho ulidhihirishwa wakati wa ziara ya Dk. Shein nchini India Febuari mwaka jana alipotembelea chuo cha ‘Barefoot” kilichoko katika Jimbo la Jajasthan.
Dk. Shein alieleza kuwa kukamilika kwa chuo hicho kutasaidia juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa mafunzo ya amali na ujasiriamali na usambazaji wa umemejua na maeneo mengine ambapo mkazo mkubwa ni kuwawezesha wanawake wa vijijini kujikwamua na umasikini.
Aliipongeza Serikali ya India kwa nia ya kuendelea kutoa ushirikiano na kuunga mkono miradi ya maji, elimu huku akipongeza hatua zinazoendelea za kutekeleza makubaliano yaliofika katika ziara yake nchini.
Naye Balozi Shaw alipongeza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya India na Zanzibar na kuahidi kuuendeleza kwa lengo la manufaa kwa pande hizo.
Balozi Shaw alisema kuwa India itahakikisha inakamilisha miradi yote ya maendeleo iliyoanzishwa kwa ushirikiano kati yake na Zanzibar kwa kutambua kuwa kukamilika kwa miradi hiyo ndio chachu ya kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano uliopo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment