Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Viongozi mbali mbali wa serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo wakiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ziara maalum,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ziara maalum na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, [Picha na Ikulu.]
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 19 Julai, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameondoka leo kwenda nchini Uingereza kwa ziara maalum ya wiki mbili.Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Dk. Shein, ambaye amefuatana na mke wake Mama Mwanamwema, aliagwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anatarajiwa kurejea nchini mara baada ya kumalizika ziara hiyo.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822


No comments :
Post a Comment