zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, July 18, 2015

KIONGOZI WA MZALENDO.NET AIELEZEA SIKUKUU ILIVYO KULE ZANZIBAR LEO!

Eid Mubarak

Written by 

Assalam alaykum warahmatul llah wabarakatuh.

Eid Mubarak, kullu jamii Zanzibar walmuslimina.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kwamba leo tumekamilisha mfungo wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Tukiwa tumo kwenye sherehe hii ya kukamilisha swaumu na tukiwa na matumaini ya kukubaliwa funga zetu kama sehemu ya ibada na nguvu kuu ya uislam, hatuna budi kuwafikia na kuwatakia kila la kheri wengi wengineo.

Sahani hapo juu zinajionyesha kwa upande wangu nilivyosherehekea Sikukuu hii kwa mwaka huu.

Hivi sasa niko mitaani kusabah ndugu na jamaa pia kuzungumza na watoto, vijana nk asubuhi hii.

Pamoja nami niko na kajana mutanakashi akiwa amevaa ile flavor ya Kizanzibar ; kanzu nyeupe, kilemba na viatu vya kubadhi.
Anasema Ramadhani ya mara hii ilikuwa kwa vile hali ya hewa haikuwa na jua kali. La kushangaza alikuwa siku zote anapenda kufutari chakula cha wali.

Amejipanga kusherehekea kwa. asibuhi kuanza kusalimia wazee wake, kupata chakula cha mchana ambacho kitakuwa Pilau na Kuku na wakati wa jioni atatembelea Forodhani.

Niko na ndugu yangu mwengine anasema Ramadhani ilikuwa nzuri haikumpa shida. Anasema mwezi mzima wa Ramadhan walikuwa wakipata na wakila rizki za halali. Anasema watu wengi walishiriki katika ibada.

Alikuwa anapendelea kula futari ya ndizi na bei ilikuwa ya afadhali. Baada ya kuamka asubuhi hii amepanga kwenda kuwatembelea dada, kaka, ami, shangazi zake na jamaa wengine.

Wakati wa mchana wametayarisha wali, mchuzi wa njegere, kuku wa kukausha, pweza. Jioni anakwenda kutembea Mnazimmoja.

Hivi ndio sikukuu ya mwaka huu inavyoendelea hapa Zanzibar.

Eid Mubarak



No comments :

Post a Comment