Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 2, 2015

Harakati za Uchaguzi Wagombea wa CCM Zanzibar

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Kibweni wakihakiki majini yao walipofika katika kituo hicho kupiga kura kumchagua Mbunge Mwakilishi na Madiwani katika Jimbo la Mtoni Zanzibar, zoezi hilo limeanza leo Zanzibar kutafuta Wawakilishi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Maofisa wa Uchaguzi wa CCM wakihakiki jina la Mwananachama wa CCM wa Tawi la Kibweni wakati wa zoezi la kupiga kura kumchagua Mbunge Mwakilishi na Diwani wa Jimbo la Mtoni.
Wananchi wa Kibweni wakiwa katika Tawi la CCM Kibweni wakisubiri kupiga kura. kuwachagua Viongozi wao. kuliongoza Jimbo la Mtoni Zanzibar.
Wananchi wa Sharifu Msa wakiwa katika Tawi la CCM Mtoni kupiga kura kumchagua Mwakilishi Mbunge na Madiwani wa Jimbo la Mtoni wakiwa katika folini kusubiri zamu zao kupiga kura tawini hapo.
Mwakilishi wa Bububu anayemaliza muda wake Mhe Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) akiwa katika kituo cha kupigia kura tawi la Mtoni akifuatilia zoezi hilo la kuwania nafasi ya kuchaguliwa kuiwakilisha CCM kugombea jimbo la mtoni.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi Tawi la CCM Mtoni akihakikiwa kabla ya kukabidhiwa kura yake kama mwanachama hai wakati wa zoezi hilo.
Mwananchi wa Shehia ya Mtoni akipiga kura yake kumchagua kiongozi amtakae

Wananchi wa Tawi la CCM Muembemakumbi wakiwa katika foleni kusubiri kupiga kura yao kuwachagua Mbunge Mwakilishi na Madiwani wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakipigia kura Skuli ya msingi muembemakumbi.
Wananchi wa tawi la CCM Muembemakumbi akitumia haki yake kumchagua kiongozi amtakae katika Jimbo la Chumbuni kuweza kuiwakilisha CCM katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu. 






















/ZanziNews

No comments :

Post a Comment