Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 2, 2015

Mawakala BVR wagoma, wadai posho ya siku nne

Wananchi wa Tabata Dar es Salaam jana wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kieletroniki (BVR) katika kituo kilichopo kwenye ofisi za Serikali ya Mtaa wa Tabata Kisiwani. Picha na Salim Shao
Dar es Salaam. Mawakala wanaoandikisha vitambulisho vya wapigakura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voter Registration (BVR), katika Kituo cha Shule ya Msingi Umoja, wamegoma kuendelea na uandikishaji kwa madai ya kutolipwa posho.
Akizungumza kwa niaba ya mawakala wenzake katika manispaa ya Kinondoni, Yusufu Msigiti alisema mkataba wao uliisha jana, lakini walipewa malipo ya siku sita badala ya kumi.
Alisema hata walipofuatilia waliambiwa wanapaswa kulipwa na manispaa au Serikali ya kata.
Hata hivyo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mabibo, Paul Ngunga alidai kuwa alikaa kikao na mawakala hao akawaeleza kuwa katika manispaa hiyo, fedha iliyotoka ni ya siku sita tu, hivyo waendelee kuwa na subira.
“Sehemu nyingine mawakala wanaendelea na kazi, hawa ndiyo hawajaelewa, wamegoma.... nimeshaleta mawakala wengine na wanaendelea na kazi ya kuandikisha wananchi,” alieleza Ngunga.
Hata hivyo, Msigiti alisema: “Hatujawahi kulipwa na watu hao, lakini tunashangaa mtendaji wa kata anatuambia tuende huko, fedha yenyewe wanayotulipa ni ndogo tunafanya kazi ngumu kuanzia saa moja asubuhi hadi saa 12 jioni.”
Msigiti alisema mtendaji huyo aliwajibu vibaya baada ya kumhoji kuhusu posho zao za siku nne ambazo hawajalipwa badala yake aliwaambia anayetaka kazi aendele na asiyetaka aache.
Mawakala hao wamemtupia lawama mtendaji huyo kwa majibu yake ilihali wana malalamiko ya msingi.
Walisema hakukuwa na haja kwa mtendaji huyo kuita polisi kwa lengo la kuwazuia mawakala hao kudai haki yao.
Wakala Peter Mnyika alisema polisi walivyofika eneo hilo walimpiga mwandishi wa habari aliyekuwa eneo hilo na kumzuia kukusanya taarifa zake.
“Alikuwa amevaa kitambulisho na alijitambulisha baada ya kuona vurugu zinazidi lakini askari mmoja wa kiume alimkunja mwandishi huyo na baada ya kuona waandishi wenzake wamefika na kamera alikimbilia ofisi ya mwalimu mkuu na hajatoka mpaka sasa,” alieleza Mnyika.
Mwandishi aliyepigwa ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema askari ndiyo wamekuwa wa kwanza kumzuia kufanya kazi yake badala ya kumpa ushirikiano.
Yusufu Kileme alikiri mtendaji wa kata kutumia lugha mbaya wakati mawakala wakidai haki yao.
Pia, alisema askari wanaofika eneo hilo wanapaswa kuangalia anafanya fujo ili wazuie, na siyo kuwa chanzo cha vurugu.
Mwenyekiti wa kata hiyo, Saimoni Ramo alisema askari walipofika aliwasihi wasitumie nguvu kwa sababu malalamiko ya vijana hao ni ya msingi.
“Askari walitakiwa kutumia busara na siyo nguvu hili ni tukio dogo, tunakoelekea ndiyo kukubwa zaidi. Sasa kama wanafanya hivi, kwenye Uchaguzi Mkuu siyo ndiyo watatuvunjavunja,” alisema Rahino.
/MWANANCHI.

No comments :

Post a Comment