Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik.
- Akizungumza jana ofisini kwake, mbali na kushikana mikono, Sadik aliwataka wananchi kuacha kunywa maji ya viroba maarufu kama “maji ya Kandoro” na juisi za mitaani ili kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huo.
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Said Meck Sadik amewataka wakazi wa jijini hilo kuchukua
hadhari za kiafya ikiwamo kuacha kusalimiana kwa kushikana mikono
kutokana na mlipuko wa kipindupindu ambao mpaka sasa umeshawapata watu
56, kati yao watatu wamefariki dunia.
Akizungumza jana
ofisini kwake, mbali na kushikana mikono, Sadik aliwataka wananchi
kuacha kunywa maji ya viroba maarufu kama “maji ya Kandoro” na juisi za
mitaani ili kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huo.
“Masuala
ya kusalimiana mikono kwa mikono katika kipindi hiki tuepukane nayo
lazima tunyanyapaliane wakati huu, ndiyo maana nilipoingia hapa
sikuwapeni mikono kwa sababu nazingatia masharti ya madaktari,”
aliwaambia waandishi wa habari.
Alisema ugonjwa huo ulilipuka Agosti 15 baada ya mtu mmoja kufariki dunia katika Hospitali ya Mwananyamala. “Hata familia yake, mke na watoto walipochukuliwa vipimo na wao walidhihirika kwamba wana maambukizi ya kipindupindu na mpaka sasa hivi bado tunao katika kituo chetu cha afya pale Mburahati,” alisema Sadik.

Alisema idadi ya wagonjwa imeongezeka
hadi kufikia 56 lakini mpaka sasa wamebaki wagonjwa 36 katika kituo
maalumu kilichofunguliwa Mbagala baada ya wengine kutibiwa na kuruhusiwa
kurudi nyumbani.
Aliwataka wananchi kuepuka kula
chakula kilichopoa na matunda ambayo hayajaoshwa. Alizitaja dalili za za
ugonjwa huo kuwa ni kuharisha mfululizo, choo kuwa cha majimaji meupe
kama ya mchele, kutapika mfululizo, ngozi kusinyaa, kiu kali, mdomo
kukauka, mapigo ya moyo kuongezeka na mwili kukosa nguvu.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Marufuku-kupeana-mikono-Dar/-/1597296/2840700/-/y5jw1w/-/index.html
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Marufuku-kupeana-mikono-Dar/-/1597296/2840700/-/y5jw1w/-/index.html
No comments :
Post a Comment