Kayombo alikwenda ofisi za CCM wilayani humo Agosti 14 na kutaka arudishiwe vifaa vya matangazo, baada ya kushindwa kwenye kura za maoni Agosti Mosi 2, mwaka huu.
Mmoja wa makada alisema Kayombo alichukua hatua hiyo akisema viongozi wa Chama wilaya hawamtaki.
Katibu wa CCM wilaya ya Mbinga, Zainabu Chinowa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wamesikitishwa na kitendo hicho.
“Tunajua kitendo cha kutunyang’anya vipaza sauti ni hasira baada ya kushindwa, kwenye uchaguzi wa kura za maoni,” alisema Chinowa.
Alipotafutwa Kayombo, alisema kuwa madai hayo siyo ya kweli na kueleza kuwa Chama kimekuwa kikiviazima vifaa vyake mara kwa mara kwa kuwa yeye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec).
“Siku za kwanza za kampeni hawakuvitumia vipaza sauti vyangu, walisema vimeharibika. Baadaye walinunua vipya na wakavipeleka majimbo ya Mbinga Mjini na Vijijini,” alisema Kayombo na kuongeza:
“Majuzi nilikwenda nikakuta havijatunzwa vizuri , nikawaambia wanirudishie vifaa vyangu.”Kadhalika, Kayombo alisema hakushindwa kura za maoni kwa kuwa matokeo ya kata mbili hayajajumuishwa.
Katibu wa CCM wa mkoa wa Ruvuma, Vellena Shumbusho, alisema amelazimika Chinowa kumkabidhi haraka Kayombo vifaa vyake anavyodai.
Alisema Kayombo alikuwa amevinunua na kuvikabidhi kwenye Chama kwa ajili ya kusaidia matangazo wakati wa kampeni za kura za maoni Jimbo la Mbinga Vijijini lilikuwa na wagombea ubunge nane waliochuana katika kura za maoni.
Martin Msuha aliyeongoza kwa kura 13,354, Kayombo (12,068), Deodatus Ndunguru (7,060), Humprey Kisika (545) na Dk. Silverius Komba (3,941).
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment