Mlezi wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Zanzibar Dkt. Mohd Makame Haji akiwakaribisha wageni walikwa katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani uliofanyika huko Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyekiti wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Zanzibar Ali Kombo Hassan akisoma risala ya vijana wa vilabu UN katika Mkutano uliofanyika Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
Mjumbe wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu Khadija Salum Khamis akitoa hutuba yake kuhusu madhara yanayopatikana kutokana na vurugu za uchauzi, katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani.
Afisa elimu ya wapiga kura kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar Juma Sanifu Sheha akitoa mada juu ya ushiriki wa vinaja katika uchaguzi wa Amani katika Mkutano wa kuadhimisha siku ya vijana Duniani uliofanyika huko Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya Vijana wa vilabu vya UN vya Elimu ya juu wakimskiliza kwa makini mtoa mada Juma Sanifu kutoka Tume ya Uchaguzi (hayupo pichani) wakati akiwasilisha.
Afisa programu ya maendeo ya Vijana mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa ofisi ya Zanzibar Aoife Spengeman akitoa shukrani kwa vijana mara baada ya kumaliza kwa Mkutano huo (kushoto) Mratibu wa vilabu vya UN Zanzibar Maalim Ame Haji Vuai. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.
/ZanziNews.
No comments :
Post a Comment