Adaiwa kuchukua fomu za vyama viwili tofauti vya CCM na ACT- Wazalendo ili kuwania udiwani.
Kwa mujibu wa Chuma, amechukua uamuzi huo kwa kile alichodai kuhujumiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kwa kumtuhumu mambo mbalimbali ikiwamo kudaiwa kuchukua fomu za vyama viwili tofauti vya CCM na ACT- Wazalendo ili kuwania udiwani hali iliyojenga chuki kwa wanachama na kuamua kutomchagua.
Alisema kutokana na hali hiyo ameamua kujivua rasmi uanachama wa CCM na kwamba atajiunga na chama kingine ambacho hata hivyo hakukitaja jina ili aendelee kuwatumikia wakazi wa kata hiyo ya Mhongolo.
“Nawashukuru wanachama kwa kumpatia ushirikiano hafifu katika mchakato wa kura za maoni kutokana na kupandikiza chuki,” alisema.
Akizungumzia madai hayo ya Chuma, Katibu wa CCM Kata ya Mhongolo, Lucas Ntwana, alisema ofisi yake haijapokea taarifa yoyote za mwanachama kujivua uanachama na kujiunga na chama kingine.
Hata hivyo, alisema ana taarifa za madai kuwa mwanachama huyo alichukua fomu mbili za vyama tofauti ili kugombea udiwani.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment