Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 31, 2015

UVCCM Washauriwa Kushawishi Wenzao Kukipatia Ushinda Chama cha Mapinduzi.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini Mbarouk Mrakib akitoa mada yake katika Semina elekezi  kwa Vijana kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyofanyika Uroa Kusini Unguja. Kulia kwake ni Mlezi wa kundi maalum na Mbunge wa Vijana Tauhida Galos na kushotoni kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Khamis Ali na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini Haji Machano Juma.  
Mlezi wa kundi maalum na Mbunge wa Vijana Tauhida Galos akitoa nasaha kwa Vijana wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini Unguja(hawapo pichani)katika Semina elekezi kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyofanyika Uroa Kusini Unguja. Kushoto yake ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini Mbarouk Mrakib,Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Khamis Ali na Katibu wa UVCCM Wilaya hiyo Haji Machano Juma
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Khamis Ali akifungua Semina elekezi kwa Vijana kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyofanyika Uroa Kusini Unguja, kulia kwake ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini Mbarouk Mrakib, Mlezi wa kundi maalum na Mbunge wa Vijana Tauhida Galos na kushoto kwa Khamis ni Katibu wa UVCCM Wilaya hiyo Haji Machano Juma. Katibu wa UVCCM Wilaya hiyo Haji Machano Juma


Baadhi ya Vijana wa UVCCM kutoka Wilaya ya Mfenesini wakifuatilia Mada kutoka kwa Viongozi wao hawapo pichani katika Semina elekezi kwa Vijana hao kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyofanyika Uroa Kusini Unguja


Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wamehimizwa kuendelea kuwashawishi WanaCCM wenzao na wale wa Vyama vya upinzani kuipigia kura CCM ili Chama hicho kiendelee kutawala Bara na Visiwani.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Umoja huo wa Wilaya ya Mfenesini Mbarouk Mrakib wakati akitoa mada katika Semina elekezi kwa Vijana iliyofanyika Uroa kusini Uguja.

Amesema Vijana ndio watetezi wakubwa wa Chama nakwamba juhudi zao zinahitajika zaidi kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kukipa ushindi wa kishindo chama hicho kuliko miaka ya nyuma.

“Tusisahau wajibu wetu ambao ni kumshawishi kila Mpiga kura bila kujalisha chama chake aipigie kura ya Ndio CCM kwani ni Chama pekee chenye Nia thabiti ya kuleta mabadiliko ya Kiuchumi” Alisema Mrakib.
Kwa upande wake Mlezi wa kundi maalum ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum Tauhida Galos Cassian amewaomba Vijana wa CCM kuwa na msimamo bila ya kuyumbishwa na Vyama vya upinzani.

Amesema vyama vyote vinakimbilia kundi la Vijana kwa vile ndio kundi kubwa na jepesi kushawishika hivyo kuwasisitiza Vijana hao kuendelea kuiamini CCM ambayo ndio Mkombozi wa Uchumi.

“CCM imefanya mengi katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Uchumi, Miundombinu na Michezo hivyo Wananchi wanakila sababu ya kuendelea kuiamini ili izidi kuleta maendeleo”Alisema Tauhida.

Akifungua Mafunzo hayo Mgeni Rasmi wa Semina hiyo Khamis Ali ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC amewataka Vijana hao kushirikiana na kuyatekeleza yale wanayoambiwa na Viongozi wao.

Naye Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini Haji Machano Juma amewaomba Vijana walioshiriki Semina elekezi kuhakikisha Wanatoa elimu kwa Vijana wengine ambao hawakushiriki Semina hiyo.

Semina hiyo ya kuwajengea uwezo Vijana hao juu ya mambo mbalimbali yanayohusu Uchaguzi na wajibu wao ili kufanikisha Ushindi kwa Chama cha Mapinduzi ilifanyika Mwisho wa Wiki katika Hoteli ya Coconut Uroa Kusini Unguja.

                   IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments :

Post a Comment