Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 17, 2015

Waliogombea Busega sasa wapinga ushindi.

  'Hatukubaliani na matokeo haya ambayo yalichakachuliwa'.

Dk. Raphael Chegeni.
Waliokuwa wagombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika jimbo la Busega mkoani Simuyu, wamepinga matokeo ya marudio ya kura za maoni, katika uchaguzi uliorudiwa Agosti 13 mwaka huu yanayoonyesha kuwa Dk. Raphael Chegeni (pichani) alishinda akifuatiwa na Dk. Titus Kamani.
 
Wagombea hao waliopinga matokeo hayo ni Nyangi Msemakweli, Robart Nyanda, Josephat Nkwabi, Desian Sweya na Igo Shing’oma kati ya wagombea nane walioshiriki kinyanganyiro hicho.
 
Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, walisema kuwa matokeo ya awali ambayo yalinyesha kuwa Dk. Kamani aliongoza kwa kura 12,896 dhidi ya Dk. Chegeni ambaye alipata kura 12,745, waliridhika nayo na walisaini, lakini walishangazwa na maamuzi yaliyotolewa na Chama ngazi ya Taifa kuwa warudie uchaguzi.
 
“Ni kweli tuliridhika kabisa na matokeo hayo ya awali, lakini hatukuelewa sababu za kurudia matokeo na tuliporudia makosa mengi yalijitokeza likiwamo suala la rushwa na upendeleo wa wazi kati ya viongozi wa wilaya dhidi ya Dk. Chegeni,” alidai Sweya.Shing’oma alidai kuwa  wanayoyatambua ni matokeo ambayo waliyakusanya wenyewe kwenye vituo ambayo yanayoonyesha Dk. Kamani aliongoza kwa kura 12,852 dhidi ya Dk. Chegeni aliyepata kura 12, 664 kabla ya yale yaliyotangazwa na Katibu wa CCM wilaya.
 
“Hatukubaliani na matokeo haya ambayo yalichakachuliwa na viongozi wa wilaya,  imani yangu Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, atatenda haki kwani tumeshampelekea malalamiko yetu,” alisema Shing’oma.
 
Hata hivyo, wagombea hao walitangaza msimamo wao juu ya kutokihama chama hicho kwa sababu mbalimbali na kudai kuwa ni chama pekee kinachoweza kuivusha nchi.
 
Mwishoni mwa wiki, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alikaririwa na vyombo vya habari akielezea kuwa malalamiko yote katika majimbo ambayo uchaguzi  ulirudiwa Agosti 13 yanafanyiwa kazi kwa kuzingatia ngazi husika hadi Taifa kabla ya kutangazwa matokeo rasmi.
 
Nape alibainisha kuwa, Kamati kuu inatarajia kutangaza wagombea ubunge wa majimbo yaliyorudiwa uchaguzi huo leo.
 
Majimbo mengine ni Kilolo, Rufiji, Ukonga na Makete.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment