Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 4, 2015

Dua ya kuiombea Zanzibar amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi


Dua ya kuiombea Zanzibar amani na utulivu wakati wa uchaguzi Wilaya ya Wete




Waumini wa kiislamu wakiwa pamoja katika dua dua ya kuiombea nchi amani wakati wa uchaguzi, iliyofanyika huko Wete Pemba. Dua ilitanguliwa na Sala ya Sunnah

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC Bw. Hamad Rashid Mohamed, baada ya kushiriki kwenye dua ya kuiombea nchi amani wakati wa uchaguzi, iliyofanyika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.

    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiongozana na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga, baada ya dua hiyo.
 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, akisoma dua kabla ya kuanza kisomo maalum cha kuiombea nchi amani, katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na: Hassan Hamad, OMKR
Waislamu mbali mbali wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo wamekusanyika katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar kwa ajili ya kuomba dua ya kuiombea nchi amani na utulivu katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Sheikh Abdallah Talib, amesema mara nyingi amani ya Zanzibar hutoweka kutokana na sababu za kisiasa hasa inapofika wakati wa uchaguzi mkuu, hivyo juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa katika kuendeleza amani ya nchi wakati wote.

Amesema suala la kudumisha amani na utulivu ni mchakato unaopaswa kuendelezwa, ili kuinusuru nchi kuingia katika machafuko yasiyokuwa ya lazima, na kwamba kila mwananchi ana jukumu la kuhakikisha kuwa amani ya nchi haichezewi.

Naye Amir wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar Sheikh Ali Abdallah amesema dua hiyo ya kitaifa imefanyika nchi nzima katika viwanja mbali mbali Unguja na Pemba.

Dua hiyo iliyotanguliwa na sala ya Alasiri viwanjani hapo, imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini ya kiislamu, serikali na vyama vya siasa wakiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Soraga, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha ADC Mhe. Hamad Rashid Mohammed.

No comments :

Post a Comment