Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka akimpatia maelekezo juu ya NEC inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo alipoitembelea kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
Vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vilivyowasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimuonyesha Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka moja ya vifaa vilivyowasili kwa ajili ya kusaidia Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015.
Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka juu ya NEC inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo alipoitembelea kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni Kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw Kailima Ramadhani.
Serikali imeahidi kuipatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi fedha zote ambazo inazihitaji kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Octoba 25 mwaka huu kutoka vyanzo vyote vya mapata. Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka amesema hayo leo alipo itembelea Tume ya Tafifa ya Uchaguzi kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari. "Changamoto ya kifedha ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa ikikabiliana nayo awali sasa haipo tena kwakuwa serikali imedhamiria kuipa NEC fedha zote ambazo inazihitaji katika kuhakikisha Uchaguzi mkuu unafanyika Octoba 25 mwaka huu. Fedha hizo zitatolewa kwa awamu, kutokana na ratiba ya tume ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa ambavyo vimeanza kuwasili , mafunzo kwa wasimamizi wa Uchaguzi na zoezi zima la Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais. Vifaa vilivyo wasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni pamoja na vitutuli[vibanda vya kupigia kura], mabango [yanayo onesha kituo cha kupigia kura.
No comments :
Post a Comment