Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 4, 2015

Lowassa ageukia chopa, Magufuli kuteka Moro leo.

Mgombea urais wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Wakati mgombea urais wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ameanza harakati za kuomba kura kwa wananchi kwa kutumia helkopta (Chopa), mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, ataanza kuuteka Mkoa wa Morogoro leo. 
 
Lowassa ambaye ameanza kampeni mikoani Jumamosi iliyopita alikuwa akitumia usafiri wa magari, huku kwa siku alifanya kati ya mikutano miwili hadi mitatu.
 
Mikoa ambayo hadi jana mgombea huyo na msafara wake walikuwa wamefanya mikutano ya kampeni ni Iringa, Njombe, Rukwa na Katavi.
 
Hata hivyo, jana Lowassa alianza rasmi kutumia chopa yenye namba 5Y-PKI  akitokea Sumbawanga mjini na kufanikiwa kufanya mikutano mitatu ya kampeni eneo la Namanyere, Nkasi na Mpanda mjini mkoani Katavi.
Katika mkutano wa mwisho Chopa hiyo ilitua kwenye Uwanja wa Kashilila mjini Mpanda huku maelfu ya wakazi wa mji huo wakishuhudia.
 
Hatua ya Lowassa kuanza kutumia chopa imekuja siku moja tu baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutangaza kuwa chama hicho kimepanga kutumia helkopta nne kufanya kampeni kuanzia wiki ijayo.Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Mpanda, alisema CCM ni chama dola na siyo cha kisiasa na ndiyo maana kimeua demokrasia nchini.
 
Mgeja alisema katika kuthibitisha kuwa CCM ni chama dola ndiyo maana wakuu wa mikoa na wa wilaya ni wajumbe wa kamati za siasa.
 
Alisema CCM ni chama ambacho kimekosa dira na mwelekeo na ndiyo maana kinashindwa kutetea masuala ya wakulima na wafanyakazi licha ya bendera yake kuwa ya jembe na nyundo.
 
“Katibu Mkuu CCM, Kinana, alishawahi kusema kuna mawaziri mizigo, kama yeye ndiyo kiongozi mkuu wa chama tawala anasema hivyo kuna chama tena hapo,”alihoji.
 
Aidha, Mgeja alipinga kauli ya mgombea urais CCM, Dk. John Magufuli, kwamba wananchi wasipoichagua CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wafadhili watasitisha kutoa misaada na hata miradi ya maendeleo inayoendelea kufadhiliwa kama vile barabara vitakwama.
 
Alisema wananchi wasiwe na wasiwasi serikali itakayoongozwa na Lowassa itakuwa makini na kamwe wafadhili hawawezi kusitisha ufadhili wa miradi ya maendeleo.
 
LOWASSA KUCHUNGUZA TOKOMEZA
Kwa upande wa Lowassa, ameahidi kama wananchi watampa ridhaa serikali yake itaunda tume kuchunguza upya sakata la Operesheni Tokomeza ili watu walioathirika kutokana na operesheni hiyo waweze kulipwa haki yao.
Lowassa 
 
Lowassa alisema amepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Katavi ambao ndugu zao waliathiriwa na oparesheni hiyo na kupoteza mifugo na ndugu zao lakini hadi sasa hawajalipwa haki zao na serikali.
 
“Nafahamu serikali iliunda tume kuchunguza suala la tokomeza lakini bado kuna malalamiko mengi ya wananchi wakiwamo wa mkoa wa Katavi ambao waliathirika, mkinichagua nitaunda tume upya ili wale ambao hawajalipwa fidia kutokana na kuathirika waweze kulipwa haraka,”alisema.
 
Kuhusu mgogoro wa shamba kati ya Kanisa la Efatha na Kijiji mkoani Katavi, alisema jambo hilo limechukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na kwamba akifanikiwa kuingia Ikulu litachunguzwa upya na kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili haki iweze kupatikana.
 
Lowassa pia alihidi serikali yake itaunda tume kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo inaendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi na kusababisha kuzuka kwa mapigano.
 
“Wenzetu wa Uganda, Kenya, Burundi wametuacha, lazima tuipeleke nchi katika maendeleo ya kasi kitu cha msingi nipeni kura nyingi niingie Ikulu,”alisema.
 
Magufuli kuiteka Moro
Baada ya ya siku kumi za milima, mabonde, barabara za lami, vumbi, njaa, jua, manyunyu ya mvua, za kutembea takribani kilomita 4,000 kutoka Dar es Salaam hadi Katavi na kuelekea Mtwara kukamilisha ngwe ya kwanza, mgombe wa urais wa CCM, Dk. Magufuli, amefanya takribani mikutano 80.
 
Zilikuwa siku za kupata ajali ndogo, magurudumu kupungua upepo na baadhi ya magari kubaki nyuma, wakati mwingine kupotea njia baada ya kuachwa.
 
Kazi hiyo leo imehamia mkoani Morogoro kwa mgombea huyo kutafuta ridhaa ya wananchi kumpigia kura za kutosha zitakazomwezesha kuingia Ikulu Oktoba 25, mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment