"Nawaombeni sana wakazi wa Mkuranga msipige kura za chuki ama hasira dhidi ya CCM; kama kuna matatizo yaliyojitokeza tutayashughulikia na kuyamaliza baada ya kumalizika uchaguzi mkuu.
Mpigieni kura nyingi mgombea urais wa chama chetu Dk. John Magufuli na wagombea ubunge na udiwani...Hao wapinzani wetu walioibukia Ukawa na kuichafua CCM nao ni sehemu ya ubovu wanaoulalamikia," alisema.
Alisema mgombea urais anayepeperusha bendera wa vyama vinavyounda Ukawa, kupitia Chadema ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Fedrick Sumaye, wanahubiri kwamba CCM ni mbovu lakini wamesahau kuwa wao ndio walioifikisha hapo kwa kuitengenezea majeraha ya kila namna.
Malima alikuwa akizungumza jana katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, uliofanyika kijiji cha Kimanzichana Wilaya ya Mkuranga.
Kwa upande wake, mgombea mwenza wa Suluhu akizungumza na wananchi hao, alisema iwapo Dk. Magufuli atapata ridhaa ya kuunda serikali ya awamu ya tano anawaahidi kujenga kiwanda cha kisasa cha kubangua korosho katika Wilaya ya Mkuranga.
"Tuchagulieni Dk. Magufuli na wagombea ubunge na udiwani ili tulete maendeleo Mkuranga. Tumejipanga na tunaahidi kujenga kiwanda cha kubangua korosho hapa kwenu. Ujenzi huu pia utafungua fursa za ajira kwa vijana lakini pia kitaongeza kipato cha wakazi wa Mkuranga na maeneo ya jirani," alisema Samia.
Alisema nia ya serikali ijayo ya CCM ni kuwawezesha wakulima wa zao hilo kufungasha zao hilo katika njia ya kisasa na kuuza kwa tija ndani na nje ya nchi.
Alisisitiza kuwa Dk. Magufuli na serikali yake atakayoiunda iwapo atapata ridhaa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu; ameahidi pia kujenga soko kuu la zao la korosho ambalo litakuwa mkombozi wa wakulima wa zao hilo nchini.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment