Akizungumza na Nipashe, Lusinde ambaye pia ni miongoni mwa makada waliopo kwenye timu ya kampeni ya Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, alithibitisha ajali hiyo kutokea katika Kijiji cha Idifu, wilaya ya Chamwino, lakini hakuna maafa yoyote yaliyotokea.
Alisema kulikuwa na jumla ya abiria watano kwenye helikopta hiyo akiwamo rubani na viongozi wengine watatu wa CCM, Wilaya ya Chamwino.
Aliwataja abiria wengine kuwa ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake UWT, Wilaya ya Chamwino, Devotha Mbogoni, Katibu Mwenezi wa wilaya, Marietha Mkuya na Mwenyekiti wa Kata ya Mvumi Mission, Mathias Lusano.
“Tulikuwa tunafanya mikutano kwenye jimbo la Mtera na baadaye ningeondoka kwenda Iringa, Njombe na Ruvuma ndivyo ilikuwa imepangwa, kwanza nilitoka Dodoma mjini mpaka Mvumi na nimetoka Mvumi nimeenda Chinoje, nikafanya mkutano nikaruka kutoka Chinoje hadi Igandu,” alisema.
Alisema baada ya kutoka Igandu aliruka kwenda Idifu ambapo wakati wa kutua rubani wao akagundua tatizo na kutua mbali na watu na baada ya kumaliza mkutano wake ndipo ndege ikashindwa kupaa.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment