Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimesisitiza kuwa havitabadili uamuzi wa kuhamasisha wafuasi wao kubaki vituoni mara baada ya kupiga kura ili kulinda zisichakachuliwe.
Akihutubia katika mkutano wa kampeni alhamisi wiki hii Kawe jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, aliwataka wafuasi wa Ukawa kutoondoka kituoni mara baada ya kupiga kura ili kuzilinda zisichakachuliwe.
Hata hivyo, baada ya kauli hiyo ya Mbowe, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva, alisisitiza kuwa Nec ndiyo yenye jukumu hilo kwa kushirikiana na mawakala wa vyama vyote.
Hata hivyo, jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, aliwasisitiza wafuasi wao wasirudi nyuma katika mchakato wa kulinda kura zao mara baada ya kupiga kura.
Mnyika aliwataka wananchi kupuuza kauli ya Lubuva, ambaye alisema wakishapiga kura warudi nyumbani.
Alisema hawategemei kuona vurugu zikitokea na endapo zitatokea zitasababishwa na uchakachuaji wa matokeo.
Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo, wafuasi wao watatakiwa kufuata sheria ya kukaa umbali wa mita 100 kwa mujibu wa sheria iliyopangwa lakini si Lubuva kukataza watu wasibaki vituoni.Akihutubia katika mkutano wa kampeni alhamisi wiki hii Kawe jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, aliwataka wafuasi wa Ukawa kutoondoka kituoni mara baada ya kupiga kura ili kuzilinda zisichakachuliwe.
Hata hivyo, baada ya kauli hiyo ya Mbowe, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva, alisisitiza kuwa Nec ndiyo yenye jukumu hilo kwa kushirikiana na mawakala wa vyama vyote.
Hata hivyo, jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, aliwasisitiza wafuasi wao wasirudi nyuma katika mchakato wa kulinda kura zao mara baada ya kupiga kura.
Mnyika aliwataka wananchi kupuuza kauli ya Lubuva, ambaye alisema wakishapiga kura warudi nyumbani.
Alisema hawategemei kuona vurugu zikitokea na endapo zitatokea zitasababishwa na uchakachuaji wa matokeo.
Aidha, alisema watakuwa na mawakala wao ambao watakuwa nje na ndani kusimamia kura zao.
Alisema ni wajibu wa wananchi kusimamia kura zao na kama Nec wana ajaenda ya siri, Lubuva aieleze kwa kuwa wameweka mambo yao kwa uwazi kuwa mpigakura ana haki ya kushuhudia kura yake na kuilinda.
Katika hatua nyingine, Mnyika alimtupia lawama Rais Jakaya Kikwete kwa kushindwa kufanikisha katiba mpya ambayo ingejibu swali la tume huru ya uchaguzi iliyotegemewa kuondoa malalamiko kuhusu uchaguzi.
Alidai kuwa kati ya watu ambao wanaiingilia Nec na kuvuruga utendaji wake ni Rais Kikwete kwani amekuwa akifanya hivyo kwa namna mbalimbali.
Alisema mambo ambayo Nec inayafanya kwa sasa yamesababishwa na rais kwa kushirikiana na chama chake kwa kuisababishia Tanzania kukosa katiba mpya ambayo kama ingekuwapo ingejibu suala la kuwa na tume huru ya uchaguzi na mifumo huru.
“Rais yeye binafsi alikubaliana na vyama kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kwamba kama hakuna katiba mpya basi walau twende kwenye uchaguzi tukiwa na marekebisho madogo ya mpito ya kuwezesha matokeo ya rais kupingwa mahakamani, kuwe na mgombea binafsi na tume huru ya uchaguzi,” alisema Mnyika.
“Kikwete alikwenda kinyume cha ahadi zake, hapakufanyika marekebisho yoyote ili katiba ibaki ilivyo, matokeo yatangazwe haraka haraka na mshindi akishatangazwa ametangazwa jambo hili halipaswi kukubalika, natoa wito kwa wapenda amani kuanzia watakaokuwa nyumbani na wale watakaokwenda kwenye tamasha la amani ambalo mgeni rasmi ni Rais Kikwete, wamuombee ili yeye na chama chake waache kuandaa mazingira mabovu," alisema Mnyika.
Alisema hawataacha kutoa matamshi mara kwa mara kwani yatasaidia kuwapo na uchaguzi ambao utakuwa huru na wenye haki na kwamba Jaji Lubuva anapaswa kuombewa ili awe na ujasiri wa kusimamia haki.
Mnyika alisema rais na wenye mamlaka wasitegemee kuipitisha Tanzania njia ambayo Kenya ilipitia ama mataifa mengine yamepitia. Hivyo Nec inatakiwa kutoa nafasi ya haraka ya kwenda kulikagua daftari na mfumo wenyewe sambamba na kushughulikia mambo mengine.
Alisema mfumo wa kujumlishia matokeo walitakiwa kutoa fursa kwa wataalam wao kwenda kuukagua lakini jambo hilo halijawekwa wazi.
Aidha, alisema wadau wakubwa wa uchaguzi ambao ni vyama vya siasa hadi sasa hawajapangiwa lini watakutana na Nec, wakati kuna malalamiko ya msingi yanayotakiwa kushughulikiwa.
Pia alisema mpaka sasa hawajapatiwa orodha ya daftari la wapiga kura ili wataalam wao waweze kuhakiki kama ilivyokuwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
“Huo ni mkakati wa kuchelewesha ili mjadala usiendelee, kila mtu asubirie siku nane kabla ya uchaguzi halafu hizo siku nane sio kwamba chama kinapatiwa madaftari ni kwamba wanakwenda kubandika majina vituoni ili kutazama jina lako na usipoliona huna la kufanya, hizo ni njama zao watueleze ni kwa nini hawataki kutoa daftari la awali na la mwisho,” alisema.
Mnyika alisema hawapo tayari kucheleweshewa kwani mambo hayo ni muhimu la sivyo wanawapa mashaka huenda pakawapo na uchakachuaji.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment